Ile filamu mliyokuwa mnaisubiri kwa hamu iitwayo “Cultural Wars” iliyoandikwa na kutengenezwa na Deogratius Mhella (Mtanzania anayeishi New York) akishirikiriana na Watanzania na Wamarekani waishio New York, New Jersey Boston na Connecticut sasa imetoka kwa mara ya kwanza na inapatikana kwenye DVD na unaweza kupata “electronic Copy” na vile vile unaweza kuiona online kupitia: www.createspace.com/405841 
 Filamu hii inazungumzia baadhi ya changamoto za kimapenzi wazipatazo vijana wa Kitanzania hapa Marekani. Na ni ya kwanza iliyochezwa na Watanzania na Wamarekani hapa New York kwa kutumia lugha ya Kiingereza. 
Baadhi ya “Actors” wa Kitanzania ni Khalifa Siwa aka “Bob”, Ibra aka “Vijimambo New York”, Akida aka “Mshenga”, Chemi Whitlow aka “Chemponda” na Isaac Kibodia aka “Father”. Wote mliosaidia katika kufanikisha filamu hii ambao hamjatajwa hapo juu, mnapewa shukrani za dhati kabisa.
 Usikose kujipatia nakala yako ya DVD kwa kuinunua au kuiona kupitia: www.createspace.com/405841

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 01, 2014

    Watanzania wenzetu wa New York tumefurahishwa na kututoa kidedea majuu. Endeleeni Kuitangaza Bongoland.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 02, 2014

    Ndugu Mhella hongera sana ... Tulikuwa wote London na sasa naona umeamua kufanya kweli... Do you remember professor Lynch? He used to say "always aspire for higher heights", You got it brother. Congratulations!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 02, 2014

    Ileteni Tanzania. Tunaisubiri kwa hamu!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 02, 2014

    Ileteni Tanzania. Tunaisubiri kwa hamu!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 02, 2014

    Tanzanians abroad must show us that even there success is not an issue. Writing and directing a movie is not easy at all. I am a movie director and I know what it means to direct a movie. So Congratulations Deo. Keep it up and release another film.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 02, 2014

    President Kikwete it would good if you embrace vijana Kama Hawa maana wanaliletea taifa la Tanzania heshima.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 03, 2014

    Nyingine mtakayofanya itakuwa vizuri mkipata actors mmoja au wawili kutoka Bongo. Hii itasaidia sana kuzidisha marketing strategy yenu Huku Bongo! Kazi nzuri mlichofanya. Nimeikubali.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 03, 2014

    Movie za Kinigeria zimetawala Bongo. Mkiendelea vizuri Mtapata soko zuri Bongo. Kama Movie za Kinigeria zinauzika Bongo kwa nini zenu zisiuzike? Nimefurahishwa na Wazo hili na kuthubutu kwenu. Mlithubutu na mkaweza. Tunawatakia mafanikio mema

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 03, 2014

    Napenda kushirikiana kwenu na Wamarekani. Kwani wao wamebobea kwenye fani ya filamu na Mkiendelea nao mtafuta mbali sana.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 03, 2014

    Asanteni sana wote kwa maneno mazuri ya kutupa moyo. Filamu ndio hiyo naomba Naomba mnunue kwa wingi. Napenda vile vile kumshukuru Issa Michuzi na globu ya Jamii kwa kutupeperushia hewani habari ya Filamu hii. Mheshimiwa Michuzi tunaomba uendelee tangazo hili na Tunakuombea mafanikio mengi katika shughuli zako za kuendekeza blogi ya Jamii. Idumu blogi ya Jamii. From cultural wars film director.

    ReplyDelete
  11. Kaka Deo, asante sana kwa nafasi uliyotupa actors waTZ USA! Ni mimi Mama Bob aka. Chemi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...