Ndugu WanaDMV, kwa heshima na taadhima nachukua nafasi hii kujitambulisha kwenu rasmi kama Mgombea wa Nafasi ya Makamu wa Raisi wa Jumuiya ya Watanzania DMV.
Nikiwa na mapenzi ya dhati kwa jamii,nimekuwa mtetezi wa haki za watoto yatima toka utotoni mwangu. Binafsi, nilijitoa kwa kidogo nilichokuwanacho na pia, nimekuwa muhamasishaji wa misaada ya elimu,chakula mavazi na malazi kwa watoto yatima. Kwa ufupi nimeona mafanikio ya kina, japo bado wahitaji ni wengi.
Vile vile, nilikuwa mstari wa mbele katika uanzishwaji wa Kikundi cha Wanawake cha Kupambana na Ukimwi “KIWAKUKI”.Chombo hiki kimedumu takribani miaka 25 na kinaendelea kusaidia wengi nchini Tanzania kikishirikina na mashirika mbali mbali duniani.
Nikiwa Mwanadiaspora nimepitia changamoto nyingi za afya na huduma zake. Jambo ambalo lilinishawishi kuingia taaluma ya afya ili niweze kuwa msaada kwa jamii. Jitihada hizi zimenipelekea kuanzisha blog yenye kutoa elimu afya kwa jamii kwa lugha ya kiswahili “NesiWanguBlogspot.com”. Nia ni kuleta mwamko katika uwanja wa afya na huduma zake.
Zaidi, nimejihusisha na zoezi la utafutaji wa Maangalizi ya Afya kwa wanaDMV. Zoezi hilo lilikuwa jaribio la ufumbuzi wa matatizo ya fya kwa Wanadiaspora. Nashukuru kwa mchango wa kila mmoja wenu na ninaomba Wanadiaspora wa vitengo vya afya kuwa mstari wa mbele katika kujali afya za jamii yetu.
Du! huyu binti wa Uru Kishimundu amenigusa kweli kweli.Hongera sana Harrieth, Keep it up. Na hao jamaa wasimpomchagua watakuwa wana jambo.Anafaa sana huyu.
ReplyDelete