Mkurugenzi Mtendaji wa Harvard Club Of Washington, Bi. Caren A. Pauley akiutambulisha umoja wa wanafunzi waliowahi soma Chuo Kikuu cha Harvard waishio Washinton Metro Area kwa Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Liberata Mulamula siku ya Jumatano July 2, 2014 umoja huo ulipotembelea Ubalozi wa Tanzania kwa ajili ya kukutana na jumuiya mbalimbali za Kitanzania na Taasisi zinazoshughulika na maswala ya Tanzania na kuweza kuongea pamoja kufahamiana na kubadilishana mawazo.
Afisa Immaculata Diyamett anayeshughulikia maswala ya Utalii kwenye Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, akiwakaribisha wageni wote Tanzania House na kuwaambia wajisikie wapo nyumbani.
Rais wa Umoja wa Wanafunzi waliosoma Chuo Kikuu cha Harvard (Harvard Club Of Washington, Bi Yi-Fun Hsueh ambaye pia ni mmoja ya waratibu akiongea machache na kumshukuru Balozi Liberata Mulamula kwa kukubali kuwakaribisha Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani kuja kukutana na Jumuiya za Kitanzania na taasisi mbalimbali kwa ajili ya kujuana na kubadilishana mawazo.
Balozi wa Tanzania nchini Marekanai Mhe. Liberata Mulamula akiwakaribisha Umoja wa wanafunzi waliosoma Chuo Kikuu Cha Harvard waishio Washinton Metro Area kikundi kinachobeba jina la Harvard Club of Washington kwenye Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani na kuwaelezea kuhusu Tanzania na vivutio vyake chini ni maelezo aliyokuwa akitoa Mhe. Balozi MSIKILIZE
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...