Hongera sana Mr. President ‘Jakaya M. KIKWETE’
“I am Moved”, sababu nikirudi nyuma kidogo katika historia ya nchi ya Tanzania mwanzoni mwa miaka ya 90 wakati sanaa ya muziki wa kizazi kipya ilipoanza kuchipuka ikifuatiwa na vita kubwa dhidi ya kukemea kijana kuwa msanii waHIP HOP nchini na sanaa hii kupewa majina ya kutisha kama muziki wa “kufoka foka, kihuni”na sanaa hii haikukubalika kabisa katika jamii ya kitanzania.
Binafsi naweza nikasema kipindi cha awamu ya 4 ya uongozi wa serikali ya Tanzania kupitia Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ‘Dk. Jakaya Mrisho Kikwete’ ndio wakati pekee ambapo wasanii na sanaa ya kitanzania inaweza kujivunia sana.
Kwanza kabisa naweza kudiliki kusema ndio wakati pekee wasanii wa nchini wameweza kutembelea IKULU ya Tanzania kuliko vipindi vyote vilivyopita na pia kuwa ni kiongozi ambae amekua na ukaribu wa hali ya juu na wasanii wa nchini. Hata mimi binafsi ambae sijawahi kupata nafasi ya kuingia IKULU, natamani ningekua msanii kipindi hichi ili niweze kupata nafasi ya kuwa na ukaribu na Rais wa nchi yangu na naamini inaleta msukumo mkubwa sana kwa vijana ambao wanafanya sanaa nchini Tanzania kwa sasa.
Nadhani Utakuwa Mmemkosea sana Mzee Mkapa kama hamtautambua mchango wake kwa wasanii maana ndiye aliyeruhusu uhuru wa video pamoja na magazeti kwa wasanii. Mkapa alifanya kazi kubwa ya kutokuzuia wasanii wa kizazi kipya kufanya mambo yao.
ReplyDelete