Jamani Watanzania wenzangu nimesikitishwa timu ya Libe na kampeni zake za uchochezi,uongo na kashfa juu yangu mimi Idd Sandaly. Najua Watanzania wenzangu tupo pamoja tangia mliponichagua kuwa Rais wa Jumuiya ya DMV na nashukuru sana kwa ukaribu na ushirikiano mnaoendelea kunipa.
Kashfa, uongo wa kutunga bila hata kumuogopa Mungu kutoka upande wa kambi ya Libe si kwamba zinanichafulia jina bali nimezileta hapa leo mjionee wenyewe kwani nyie ndio wapiga kura na nani mnayemtaka awe Rais wenu ni chaguo lenu.
Mimi tayari mmeisha fahamu kazi yangu tangia nilipokuwa TAMCO na kwa jinsi ya ufanisi wangu TAMCO baadhi ya Watanzania na marafiki zangu walinishauri nigombee Urais wa Jumuiya ya Watanzania DMV.
Si busara hata kidogo kama haya yanahusisha kampeni.....ebu jaribuni kua na staha na kuhifadhiana kidogo...ubinadamu pia wahitajika....kumbukeni mnatazamwa na kufuatiliwa nyendo zenu na wengi...ebu onesheni ukomavu japo kidogo.
ReplyDelete