Vijana wa Kitanzania watatu wajulikanao kama 3G, wako mbioni kuachia singo yao ya kwanza, "Mrembo wa Kiafrika". Vijana hawa, ambao wali-rekodi singo hiyo mwaka jana ni G Fullah, Frankie G na Oz Bitala.
Hivi sasa wimbo huo, ambao pamoja na harmony na kuchana, una mandahari ya zilipendwa kama za Miriam Makeba na Abeti Masikini. Wimbo una ladha tofauti kidogo, na ni mziki ulioyotulia ukiambatana na acoustic guitar pekee.
Tafadhali sikiliza track hii, alafu tungependa kujua maoni yenu: je, mnaionaje kwa soko letu hili la kibongo? Ahsanteni! Download free MP3 hapa!
Joett Music - 3G Management
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...