Na
Sultani Kipingo

Hadhithi ya filamu hiyo ya
La Dolce Vita inamhusu mwanahabari mchunguzi aliyeitwa Marcello (muigizaji
akiwa Marcello Mastroianni) na mpiga picha wake aliyeitwa Paparazzo (muigizaji
Walter Santesso). Ingawa bado kuna ubishi wa maana ya jina “Paparazzo”, lakini
mfanano wake na jina la mbu mkubwa aitwaye Papataceo kwa lugha ya Kitaliani,
ilileta maana kwa kulinganisha maneno ya producer Fellini mwenyewe kwenye
taarifa aliyotoa wakati huo.
“Jina Paparazzo kwangu mimi
ni kama mbu anayeruka huku na kule
akitafuna watu walio kwenye starehe zao”, alisema Fellini, na kuachia mchoro wa
aina ya mtu asiye na mifupa (angalia picha hapo juu kulia) akiwa ameshika kamera ambayo flashi
yake inawaka, akimaanisha kwamba paparazzi, kama walivyo mbu, ni wadudu
wasumbufu.
Baada
ya filamu ya La Dolce Vita kuzinduliwa huko Italy, neno “Papaparazzi likawa
linafananishwa na wapiga picha za udaku waliokuwa wakiwinda nyota mbalimbali wa
filamu na watu maarufu na kuwaanika magazetini.
Hata hivyo, Fellini alisema yeye hakuwa anawaiga hao wapiga picha za
udaku, bali alidai yeye anachofanya ni kuyaingiza magazeti katika filamu,
wakati stori zake zilizohusu maisha ya kuponda raha wanayoishi nyota wa filamu
ziliuza sana magazeti ya udaku.
Hapana
shaka kwamba kuingia kwa neno Paparazzi katika lugha ya Kiingereza kunatokana
na hiyo filamu ya La Dolce Vita, pale ilipozinduliwa nchini Marekani huo mwaka 1961. Na lilikuwa ni jarida maarufu la
Time Magazine lililowezesha jina hilo la Paparazzi kupata umaarufu na kuwaganda
wapiga picha wa kujitegemea waliokuwa wakisaka habari za udaku za nyota wa
filamu.
Makala ya jarida hilo iliyokuwa na kichwa cha
habari cha “Paparazzi on the Prowl” (yaani paparazzi mawindoni), pamoja na
picha ya wapiga picha kibao waliokuwa wamezuia gari la Binti Mfalme mmoja
aliyekuwa ziarani Rome, ndiyo vilivyokoleza moto.
Makala
hiyo ilikuwa inazungumzia jinsi kundi la wapiga picha wa kujitegemea
walivyokuwa kama mbwa mwitu mawindoni, wakipita huku na kule kuwinda watu wenye
majina makubwa katika jamii, kuwapiga picha wakipinda raha na kuwaanika kwenye magazeti ya udaku.
Paparazzi wa Italy wakiwa kazini...
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...