Wachezaji wa timu zote mbili Miembeni Fc na Bilele Fc wakisalimiana kabla ya Mtanange kuanza jioni hii katika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
Kikosi cha Timu ya Miembeni Fc
Mabingwa watetezi wa kombe la KAGASHEKI, Bilele Fc, wamefungwa leo na Timu ya Miembeni Fc bao 2-1 kwenye mtanange uliopigwa dakika 120, dakika 90 za mchezo huo zilimalizika kwa kutoshana nguvu kwa bao 1-1 katika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
Timu ya Bilele Fc ndio walianza kupata bao la mkwaju wa penati katika dakika ya 62 kupitia kwa Fikiri David na Miembeni Fc wakasawazisha bao hilo ndani ya dakika moja na Rashid Mandawa kupita katika dakika 63 baada ya mpira kuanza kati na kufanya shambulizi.
Dakika 90 zilimalizika na kwenda katika dakika za ziada na katika dakika ya 105 Miembeni walifanikiwa kupata bao la ushindi na mtanange kumalizika. Mtanange huu pia haukuweza kumalizika vyema kwani wachezaji wawili wa Miembeni Fc wameoneshwa kadi nyekundu 2 na kucheza pungufu katika dakika za mwishoni kwa kufanya makosa tofauti tofauti.
Ushindi huu unawapeleka Miembeni Fc hatua ya Fainali wakisubiri mshindi wa kesho kati ya Kitendaguro Fc na Kagondo Fc.
Bilele Fc wao wanasubiri atakayefungwa kesho kati ya Kitendaguro na Kagondo ili waje wakutane kutafuta mshindi wa tatu.
Fikiri David wa timu ya Bilele Fc akimfunga kipawa wa Miembeni Samwel Geofrey kwa Mkwaju wa penati katika kipindi cha pili dakika ya 62.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...