Jaji Chang-ho Chung akimweleza jambo Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. John Haule akizungumza na Jaji Chang-ho Chung, Mgombea wa Nafasi ya Jaji katika Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC) kutoka Jamhuri ya Korea ambaye alimtembelea Ofisini kweke tarehe 11 Julai, 2014.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. John Haule akizungumza na Jaji Chang-ho Chung, Mgombea wa Nafasi ya Jaji katika Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC) kutoka Jamhuri ya Korea ambaye alimtembelea Ofisini kweke tarehe 11 Julai, 2014. Jaji Chang-ho Chung ambaye kwa sasa ni Jaji wa Kimataifa chini ya Umoja wa Mataifa katika Chemba Maalum za Mahakama nchini Cambodia ni mmoja wa Wagombea wanaowania nafasi sita za Majaji katika Mahakama ya ICC ambao uchaguzi wao utafanyika Mjini New York, Marekani mwezi Desemba 2014 wakati wa Kikao cha 13 cha Nchi Wanachama waliosaini Mkataba wa Rome ulioanzisha ICC.
Jaji Chang-ho Chung akizungumza huku akisikilizwa na Katibu Mkuu na wajumbe wengine akiwemo Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Irene Kasyanju (wa kwanza kulia)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...