Wakiwa wenye Nyuso za Furaha.Watangazaji mahiri wa Radio na Televisheni,Bi.Regina Mwalekwa aliyekuwa mtangazaji wa Radio One na baadae akahamia Clouds FM/TV na sasa amejiunga na Shirika la Utangazaji la BBC akiwa na mtangazaji mwenzake kutoka kituo cha televisheni cha ITV/Radio One Bi.Fatma Almas Nyangasa,kama walivyonaswa na Camera ya Globu ya Jamii ndani ya viwanja vya maonyesho ya Saba saba yanayoendelea hivi sasa jijini Dar.Bi Regina Mwalekwa kwa sasa sauti yake itakuwa ikisikika rasmi ndani ya BBC.Globu ya Jamiii inamtakia kila lakheri katika kituo chake kipya cha kazi.
Bi.Regina Mwalekwa akifanya mahojiano na mmoja wa washiriki wa maonyesho ya biashara ya Kimataifa ya Saba saba yanayoendelea katika viwanja vya Mwal.Julius Nyerere,jijini Dar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Kila la kheri Regina kwani hatua moja huvuta nyingine

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 04, 2014

    nakutakia kila la kheri katika kituo chako kipya cha kazi. nadhani halo panakufaa zaidi.

    ReplyDelete
  3. Kila la kheri dada...nilijiuliza kwann hukuwa huku kitambo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...