Maelezo ya picha;Makamu mwenyekiti Uenezi CHADEMA kanda ya Magharibi Deogratius Liyunga akiwa amelazwa katika Hospital ya Mkoa wa Kigoma(Maweni)baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana(Picha na Editha Karlo).

Na Editha Karlo, Kigoma.

WATU wasiojulikana wamemvamia na kumpiga pamoja na kumjeruhi sehemu mbalimbali za mwili kwa kutumia vitu vyenye ncha kali Makamu Mwenyekiti wa uenezi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kanda ya Magaharibi,Deogratius Liyunga na kupelekea kulazwa katika Hospita ya Mkoa wa Kigoma (Maweni).

Tukio hilo limetokea jana majira ya  saa tano usiku katika eneo la Mlole Manispaa ya Kigoma Ujiji,wakati kiongozi huyo akiwa njiani kurudi nyumbani kwake akitokea eneo la Mwanga kuangalia mechi za  kombe la Dunia.

Akiongea na mtandao huu wodini na alipolazwa juu ya tukio hilo,kiongozi huyo alisema kuwa alibakiza hatua 25 iliaweze kuingia nyumbani kwake ghafla walitokea watu wanne,mmoja alimvamia na kumkaba shingo huku wale wengine wakimshambulia kwa kisu,nyembe na ubao.

Alisema mbali ya watu hao kumpiga na kumjeruhi lakini walimpora fedha kiasi cha shilingi 63,000 ingawa hawakufanikiwa kumpora simu yake ya mkononi iliyokuwa mfukoni.

Baada ya watu hao waliomvamia kuondoka alifanya mawasiliano kwa watu wake wa karibu wakiwemo wanachama wa CHADEMA ambao walifika eneo la tukio na kumkimbiza Hospital kwaajili ya matibabu.

 Makamu Mwenyekiti alisema kuwa tukio hilo lililomkuta linahusiano mkubwa na masuala ya kisiasa kwani kabla ya tukio hilo amekuwa akipokea ujumbe mfupi wa maneno ya vitisho  kwenye simu yake ya mkononi kutoka kwa watu wanaodaiwa kuwa ni wananchama wa chama kipya cha ACT.

Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Kigoma,Frasser Kashai alipopigiwa simu na mtandao huu kuthibitisha juu ya tukio hilo alisema hana taarifa zozote kuhusiana na tukio hilo.

''Mimi hiyo taarifa sijaipata ofisini kwangu bado ndo nina isikia kutoka kwako ngoja nifuatilie nitakujulisha''alisema Kashai.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 06, 2014

    Ankali rekebisha kichwa cha habari. Hakuna mkoa wa Kigomba

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...