Mwina Kaduguda Mtunzi wa kitabu cha "HISTORIA YA SIMBA" akielezea kwa kina Magumu gani amepitia wakati anaanza kuandaa kitabu hicho,Wa kwanza Kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Juma Nkamia na Katikati ni Mkurugenzi wa Mkuki na Nyota Bwana Mkuki Bgoya ambao ndio wachapishaji wa kitabu hicho.Akielezea kwa ufupi Mwina Kaduguda amesema kwamba Dhumuni kubwa la Kutunga kitabu hicho ni kutaka kutunza historia ya soka ya Timu hiyo isipoteee ili iweze kusomwa kizazi na kizazi.




 Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Juma Nkamia Akijiandaa kukata utepe ili kuweza kuzindua rasmi kitabu hicho cha historia ya Simba,Wanaoshuhudia kulia ni mtunzi wa kitabu hicho Mwina Kaduguda akifuatiwa na Bwana Mkuki Bgoya mkurugenzi wa Mkuki na Nyota Ambao ndio wachapishaji wa kitabu hicho
Mkurugenzi wa Mkuki na Nyota Bwana Mkuki Bgoya  Akielezea namna walivyochapa kitabu hicho na ubora wake .
 Mjumbe wa kamati ya Utendaji Klabu ya Simba Bwana Collin Frisch akiongea kwa niaba ya Rais wa Simba,ambapo amempongeza sana Mwina Kaduguda na kusema ameiweka Klabu ya Simba kwenye Kumbukumbu muhimu sana kwenye soka la Tanzania hivyo inatakiwa aungwe mkono kwa nguvu zote.
 Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Juma Nkamia akitoa neno kumpongeza Mwina Kaduguda  kwa kufikiria mbali sana kwa kuweka soka la Tanzania kwenye maandishi namna klabu ya simba ilivyoanza,Akaongeza kuwa Klabu za soka Tanzania zinatakiwa kuwa na watu kama Mwina Kaduguda ili kuleta maendeleo ya soka.Naibu waziri pia akasisitiza ni wakati wa kila mwanachama kujituma kwa bidii na kuacha kukaaa kwenye korido za Klabu na kupiga Zoga.
Mwina kaduguda Mtunzi wa Kitabu cha "HISTORIA YA SIMBA" Akimkabidhi  Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Juma Nkamia Zawadi ya Kitabu ambayo ameomba apelekewe Rais Jakaya Mrisho Kikwete. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Kwa wanaohitaji kununua kitabu hiki kwa jumla au rejareja wasiliana na TPH Bookshop mtaa wa samora Dar es salaam (+255-687-238-126) au TPH Bookshop UDom Jengo la Chimwaga, Dodoma (+255-755-891-554, +255-685-233-753). Bei ya kitabu kwa rejareja ni sh 15000/= Tu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...