Na Sultani Kipingo
Kocha mpya wa Manchester United Louis van Gaal ameongea na wanahabari kwa mara ya kwanza leo, akisema kuwa klabu hicho cha Old Trafford ni kikubwa duniani isipokuwa inabidi wajipeleleze upya kufuatia kuboronga katika msimu uliopita.
"Msimu uliopita mmemaliza ligi mkiwa nafasi ya saba kwa hiyo nyie sio klabu kubwa duniani. Mnahitaji kujidhihirisha wenyewe, ingawa dunia nzima wanazungumzia Manchester United - hiyo ndio tofauti", alisema.
"Hii ni changamoto kubwa na ndio maana nikachagua klabu hii. Nimefundisha Barcelona, Ajax na Bayern Munich ambazo zote ni namba moja nchini kwao. Sasa niko Manchester United ambayo ni namba Moja England.
"Sijawahi kufanya kazi katika ligi kuu ya England na hilo ni changamoto nene. Nilipofanya kazi Barcelona, ilikuwa ligi bora. Nilipofanuya kazi Germany,nako ilikuwa ligi bora. Sasa nafanya kazi hapa penginepo hii ndiyo ligi bora.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...