
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Uwekezaji na Uwezeshaji ambaye pia ni Mlezi wa Chama cha Makatibu Muhtasi Tanzania (TAPSEA),Mh. Dk. Mary Nagu akihutubia wakati wa ufunguzi wa Kongamano la nne la Makatibu Muhtasi Tanzania,leo Julai 11,2013 jijini Mwanza.Mh. Nagu katika hotuba yake,amesema atawasimamia Makatibu hao na kuhakikisha wanaanzisha Benki yao ambayo itawawezesha kuweka abiba zao na kukopeshana pia.

Mgeni Rasmi katika Kongamano la Makatibu Muhtasi Tanzania na Mshauri wa Mambo ya Kisheria wa TAPSEA,Naibu Waziri wa Katiba na Sheria,Mh. Angela Kairuki akitoa hotuba yake katika ufunguzi wa Kongamano la nne la Makatibu Muhtasi Tanzania,leo Julai 11,2013 jijini Mwanza.Mh. Kairuki amewahimiza Makatibu Muhtasi hao kuhakikisha wanaudumisha na kuulinda umoja walionao,kwani umoja ndio msingi wa maendeo.
Mwenyekiti wa Chama cha Makatibu Muhtasi Tanzania,Bi. Pilli Mpenda akisoma hotuba yake kwenye ufunguzi wa Kongamano la nne la Makatibu Muhtasi Tanzania,leo Julai 11,2013 kwenye hoteli ya Malaika,jijini Mwanza.
Washiriki wa Kongamano la nne la Makatibu Muhtasi Tanzania kutoka maeneo mbali mbali wakifatilia mada mbali mbali.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...