Katika biashara zinazokua kwa kasi duniani ni biashara ya bima inayofuata maadili ya ki- Islam inayojulikana kama ‘Takaful’.
Misingi ya bima inayofuata maadili ya ki - Islam ni ushirikiano wa pande zote zinazohusika ktk biashara hiyo. Washiriki wote katika Takaful watashirikiana katika faida na hasara, kwa mfano, yoyote atakaenunua bima hiyo atakua ni kama mjasiri mali (investor) sambamba na yule anaendesha biashara hiyo (the takaful operator) na pande nyingine zitakazohusika kama vile share-holders.
Kama biashara hiyo ikipata faida katika kipindi cha muda fulani ambao sana ni mwaka mmoja, faida hiyo inagawiwa kwa wote wanaohusika kama ilivyotokea nchini Kenya mwaka jana ambpo bima hiyo ilishaanza sio chini ya miaka mitatu sasa.
Utaratibu wa kugawana faida na hasara haupo kataka bima ya kawaida ambapo faida hiyo inachukuliwa na muendesha biashara hiyo hata kama mwenye bima hiyo hakudai chochote kwa muda wa mwaka mzima.
Moja katika uadilifu wa bima hiyo ni ule uhakika wa kuwa faida itakayogawiwa kwa washiriki haikadiriwi kwa kiwango maalumu mpaka itakapopatikana bali itategemea faida iliyopatikana. Kwa maelezo zaidi kuhusu maswala mazima yanayohusiana na Uchumi, benki, na bima inayofuata maadili ya ki- Islam tembelea http://ijuebenkyakiislam.blogspot.com
Ni hatua nzuri kufikiwa tunashukuru kwa elimu nzuri na adimu
ReplyDeleteTugawane faida sio hasara,loss keep it .
ReplyDeleteAnonymous no 2
ReplyDeleteBiashara yoyote yenye kuchunga uadilifu ni ile ambayo ina baadhi ya majukumu ambayo mfanyabiashara anatakiwa ayakubali. Hasara ni sehemu ktk biashara ya aina yoyote na ndio maana riba ni mbaya kwakua hasara anaibeba mmoja tu ktk washirika na hivyo kuumia sana. Matokeo ya kukosekana uadilifu na kuumia kwa mmoja jamii inaathirika kwa kupatikana watu wenye kujilimbikizia mali nyingi wakati wengine ni maskini sana matokeo yake vitu kama uhalifu vinaongezeka. Inazuiya vlevile baadhi ya wenye kujilimbikizia mali kwa njia kama hizo kutotumia vipaji vyao ktk mambo ambayo jamii ingeweza kufaidika. Kwa maelezo zaidi wasiliana na www.ijuebenkyakiislam.blogspot.com.