MWANAMKE mkazi wa kijiji cha Ikandamoyo, wilayani Katavi, Veronica Saleh ‘Mama Kaela’ (50), amefanya uamuzi adimu wa kuolewa na wanaume wawili ambao anaishi nao kijijini hapo.
Kijiji hicho kipo umbali wa takribani kilometa 30 kutoka mjini hapa katika Jimbo la Katavi linalowakilishwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
Pamoja na ndoa hiyo iliyowezeshwa na mume mkubwa kukubali kuishi na mume mdogo, imeelezwa kuwa mwanamke huyo ndiye ‘aliyewaoa’ wanaume hao kwa zaidi ya miaka saba sasa, huku akiwa na amri kuu katika nyumba, kama ilivyo katika ndoa za kawaida.
Wanaume hao ni Paulo Sabuni ‘Baba Kaela’ (60) ambaye ndiye mume mkubwa na Arcado Mlele (45) ambaye ni mume mdogo.
Taarifa za kuwapo kwa ndoa hiyo ya aina yake, ziliifikia Globu ya Jamii na kufanyiwa uchunguzi kwa zaidi ya wiki tatu, na hatimaye katikati ya wiki hii, wahusika walikubali wao wenyewe kuzungumzia suala hilo. Kwa mujibu wa maelezo ya mwanamke huyo ambaye alionekana kuwa msemaji wa familia hiyo, yeye na mumewe mkubwa, walifika kijijini hapo miaka 24 iliyopita, wakitoka kijiji cha Usumbwa mpakani mwa Chunya, Mbeya na Tabora.
safi sana, maana watu wamezoea kuwa haja kubwa anaenda kuku tu, bata akienda wanaipa jina jipya eti kuendesha. mwanaume akiwa na wake wawili ni uke wenza, na inakubalika akifanya mwanamke eti ni polyandry na ni kosa la jinai , wapi usawa?
ReplyDeleteSAFIIIII! I absolutely love this woman. Power to women.
ReplyDeletemama wa katavi, nafurahi umefungua njia
ReplyDeletehabari hii ya muda mrefu,ilitoka kwenye mitandao mwaka jana.admin,kuwa current na matukio
ReplyDeleteKweli shetani ana nguvu na wafuasi wa kutosha! Unaweza kujipima mwenyewe hapahapa duniani kama wew una matendo ya kupata pepo au moto kwa Mungu
ReplyDelete