

Mwanamuziki huyo aliyekuwa maarufu zaidi duniani kama Mfalme wa Pop hadi anakufa mwaka 2009, alifika nchini akiwa balozi wa ziara ya Umoja wa Mataifa na akapokelewa kiserikali na Waziri wa Mambo ya Nje wakati huo, hayati Hassan Diria (juu kushoto).
Katika ziara yake hiyo ya siku mbili nchini, alikutana na Rais Ali Hassan Mwinyi. Kesho yake alitembelea shule maalum ya watoto yatima na wenye mtindio wa ubongo iliyopo Sinza.
Ndege yake iliyokuwa na watu takriban 60 ilishindwa kwenda mbugani Ngorongoro alikotaka kwenda. Na yeye alikuwa hawezimkupanda ndege ndogo, hivyo akaishia Dar es salaam.
Sehemu ingine aliyotembelea na kuacha gumzo ni jumba la sinema la Empire mtaa wa Azikiwe ambako aliingia katika duka la kukodi mikanda ya sinema. Naye alibeba mikanda kama 10 hivi ya vikatuni, ikiwemo ya Tom and Jerry.
One word michuzi, ASANTE
ReplyDeletemichael alipotua airport alitaraji kupanda rolls royce ambalo halikuwepo. hivyo badala yake alipanga ktk nissan patrol ambapo alikaa kiti cha nyuma pamoja na katoto kamoja ka kidhungu. Hakutaka kupanda benz lililokuwepo pale
ReplyDeleteHivi mlimualika wa kazi gani wakati aliukana uafrika na kujibadili kuwa mzungu?
ReplyDelete