Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 22, 2014

    Mtaalamu wa anga, jana tarehe 21 julai 2014 huku ulaya ya Kaskazini hapa nchini Iceland usiku wa manane tumeweza kuuona mwezi mchanga sasa hii inasababishwa na nini haswa?

    ReplyDelete
  2. Asante sana kwa swali lako la kusisimua akili. Mwezi hubadilika umbo siku hadi siku kwa mzunguko wa kila mwezi.

    Mwezi ulioona usiku wa manane una umbo kama ule wa Mwezi mchanga, lakini hasa ni Mwezi wa uzeeni ambao unaashiria kumalizika kwa mwezi.

    Mwezi huitwa mchanga ukiwa umejitokeza tu angani mara tu baada ya kuchwa kwa Jua wakati wa magharibi.

    Tukirudia Mwezi ulioona wewe usiku wa manane utaendelea kukaribia Jua wakati wa alfajiri. Siku ya Jumapili Mwezi utalinga na Jua na saa chach baadaye utajitokeza juu ya Jua kama Mwezi mwandamo mara tu baada ya Jua kutua wakati wa magharibi.

    Kwa vilie Mwezi utakuwa umepata masaa chache tu kusogea, hautakua juu sana na tunaweza kushindwa kuuona siku ya Jumapili.

    Ninatumaini umeweza kuelewa Mwezi ulioona na kulinganisha na Mwezi mwandamo.

    Asante, Jiwaji

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 23, 2014

    Mtaalamu Jiwaji,

    Asante kwa majibu yako mazuri ya kutuelimisha kuhusu elimu ya anga hususan mwezi mchanga na mwezi mzee.

    Nimeuangali mwezi tena usiku wa manane 22/07/2014 huku ulaya ya Kaskazini na kuona mwezi unazidi kuwa mdogo zaidi a.k.a unazeeka kama maelezo yako nikiufananisha na jana 21/07/2014 na pia unatokomea kuelekea kaskazini yetu hapa Iceland.

    Shukrani mtaalamu N.T Jiwaji na pia Globu ya Jamii kutupatia sehemu ya kuuliza wataalamu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...