Waziri wa Ujenzi, Dkt. John P. Magufuli amewataka wakazi wa Iramba na Majita kutunza kivuko kipya cha MV Mara ili kiweze kuwasaidia katika kuinua uchumi wa maeneo hayo.
Waziri Magufuli alitoa tamko hilo jana kabla ya kuzindua kivuko hicho kipya katika kijiji cha Iramba wilayani Bunda mkoani Mara. “Ndugu zangu wa Iramba kitunzeni kivuko hiki kwani ni mkombozi mkubwa katika kuwaletea maendeleo yenu pamoja na maeneo ya jirani” Alisema Waziri Magufuli Pia Waziri Magufuli aliwaasa wavuvi kutotega nyavu kwenye njia za kivuko ili kiweze kudumu kwa muda mrefu kwani kwa kufanya hivyo watasababisha injini za kivuko hicho kuharibika mapema.
Aidha Waziri Magufuli aliwapongeza Mbunge wa Mwibara Kangi Lugora pamoja na Mbunge wa Musoma vijijini Nimrodi Mkono kwa juhudi zao zilizochochea kupatikana kwa kivuko hicho.
Aidha, Dkt. Magufuli alisema kuwa kivuko hicho chenye uwezo wa kubeba tani 25, yaani magari manne 4 na abiria 50, kitaokoa maisha ya wananchi wengi ambao walikuwa wanapata adha kubwa ya usafiri kutokana na kukosa usafiri wa uhakika ambao ulikuwa unahatarisha maisha yao.
“Nimeambiwa hapa nauli ilikuwa Shilingi 2000/= kuvuka upande wa pili kwa kutumia boti za watu binafsi lakini kwa kivuko hiki natangaza rasmi kuwa nauli kwa kivuko chetu kipya ni shilingi 500/= tu, na wanafunzi waliovaa sare watapanda bure, watoto sh.100” Alisema Waziri Magufuli. Dkt.Magufuli aliongeza kuwa nauli za magari na mizigo zitapangwa na Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA ambao ndio wasimamizi wa kivuko hicho.
Aidha, Waziri Magufuli aliongeza kuwa Serikali itaendelea kuboresha miundombinu bila kuangalia itikadi zozote za kisiasa. Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wakazi wa kijiji cha Iramba, walisema kuwa walikuwa wanapata taabu sana ya usafiri kwani ilikuwa inawalazimu kuvuka kwa mitumbwi ambayo ilikuwa inahatarisha maisha ya wakazi wa maeneo hayo.
WAZIRI WA UJENZI DKT. JOHN POMBE MAGUFULI KATIKATI AKIKATA UTEPE KUASHIRIA UZINDUZI WA KIVUKO KIPYA CHA MV MARA KITAKACHOTOA HUDUMA KATI YA MAENEO YA IRAMBA BUNDA NA MAJITA MUSOMA VIJIJINI. KUTOKA KUSHOTO NI KAIMU MKUU WA MKOA WA MARA MHANDISI EVARIST NDIKILO AKIFATIWA NA MBUNGE WA JIMBO LA MWIBARA ALPHAXAD KANGI LUGORA, WENGINE KUTOKA KULIA NI KATIBU MKUU WA WIZARA YA UJENZI MHANDISHI MUSSA IYOMBE AKIFATIWA NA MBUNGE WA MUSOMA VIJIJINI NIMROD MKONO PAMOJA NA MWENYEKITI WA CCM MKOA WA MARA CHRISTOPHER SANYA.
WAZIRI WA UJENZI DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AKIBONYEZA KITUFE CHA KIVUKO CHA MV MARA KUASHIRIA KUKIZINDUA RASMI KWA AJILI YA KUANZA KUTOA HUDUMA KATI YA MAENEO YA IRAMBA NA MAJITA KATIKA WILAYA MBILI ZA BUNDA NA MUSOMA VIJIJINI.
WAZIRI WA UJENZI DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AAKIFURAHIA JAMBO NA MWENYEKITI WA BODI YA TEMESA BALOZI HERBERT MRANGO HUKU MBUNGE WA MUSOMA VIJIJINI NIMROD MKONO ALIYESSIMAMA KULIA NA MBUNGE WA MWIBARA KANGI LUGORA WAKWAANZA KUSHOTO WAKIANGALIA.
Wow, nimetoka mbali sana. Hapo ndio nyumbani kabisa. Hatua imepigwa japo taratibu. Nilikuwa navuka hapo kwa mitumbwi wakati niko mtoto kwenye miaka ya 80 na 90 - kutoka Mugara/Isanju (Iramba) na kwenda Chitale (Majita). Sasa hivi kuna feri? Siamini. Mbarikiwe sana. Sasa tunaomba lami angalau kutoka Bunda hadi Kisorya.
ReplyDeleteNamuona mtu na mwalimu wake,Waheshima Kangi Lugola na Magufuli.(Kumb..Sengerema Seconadary School)
ReplyDelete