Kwa mujibu wa mdau aliyeshuhudia tukio lote hilo live anatupasha:
Ishu ilikuwa hivi, kuna gari ndogo ilikuwa inatokea njia ya Kawe kwenda Shopperz au ilikuwa inaelekea mjini kwa kutumia hii njia ya Mwai Kibaki road. Hiyo gari ndogo ilipofika Maeneo ya Million Hairs Salon jirani kabisa na Regency park hotel ikakwama kwenye foleni ndefu sana. Nyuma ya hiyo gari ndogo kulikuwa na magari mengine yameunga hiyo foleni.
Gari ya magereza ikiwa na wafungwa ilikuwa ni kama ya sita au ya nne nyuma ya hiyo gari ndogo mara ghafla tukasikia puuu! puuu! pooo! poooo! poooo!  kama risasi 6 au 8 hivi - kumbe ile gari ndogo inavyosemekana ilikuwa imebeba kiasi kikubwa cha pesa na hakukuwa na escort yoyote. 
Majambazi wakiwa kwenye pikipiki waliifuata ile gari pale kwenye foleni wakamuamrisha yule jamaa atoe fedha na jamaa akaachia mkwanja. 
 Sasa lile gari la magereza kwa vile liko juu sana kama gorofa askari wake wakaiona hiyo inshu live. Sasa ile wanajiandaa tu na mabunduki yao majambazi nayo wakashitukia mchezo na wakaanza wao kuwashambulia kwa risasi wale askari magereza. Askari magereza ile wanajiandaa kujibu mapigo tu majambazi haooooo wakawasha pikipiki na kuondoka kwa speed ya 220. Kiukweli ilitisha na watu waoga kama mimi nilikimbilia kujificha sehemu. Yaani ilikuwa kama Movie (ya ulaya, sio Bongo Movie).
  Sehemu ya kioo cha pembeni cha karandinga la Jeshi la Magereza baada ya kushambuliwa kwa risasi na watu wanaodhaniwa kuwa majambazi  leo katika barabara ya Mwai Kibaki jirani na Mayfair Plaza jijini Dar es salaam. 
 Wapita njia  wakiwa wamelizungika karandinga la Magereza baada ya kushambuliwa. 
Foleni ilikuwa kali mahali hapo kwa masaa kadhaa kabla karandinga halijaondolewa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 02, 2014

    sasa tumekwisha!!!!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 03, 2014

    Hao majambazi yanataka kuiba wafungwa??? au Wafungwa walikula dili na watu ili watoroke?

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 03, 2014

    majambazi inaonekana wanafahamu issue nzima, sidhani kwamba waliotea tu kuwa hilo gari lina hela.Wasakwe wakamatwe. Sasa hizi foleni ni balaa, jamani tunahitaji doule carrier with 6 lanes, nashangaa bado njia mpya zinajengwa single carrier with 4 lanes. Maana foleni hizi sasa zina tu cost hata pakitokea moto, au gari la ambulance au issue kama hiyo ya kufukuza majambazi njia ya kupitia hamna. Muda unao potea barabarani ni mwingi mmno lazima uta athiri uchumi wa nchi.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 03, 2014

    Nadhani askari wetu inabidi warudi shule tena kujifunza techniques namna ya kuwa quick realising a danger and how to swiftly act upon it. Siamini kuwa wale majambazi walifanikiwa kukimbia pamoja na kuwepo basi zima lenye askari walikuwa on the scene wakishuhudia tukio zima. Bunduki zao zilikuwa wapi? Inatia aibu..na inaonyesha jinsi gani hiki kikundi kimebobea kwenye uhalifu wa namna hii. Wangeweza kumkamata mmoja wao tu kikundi kizima kingesambaratika.. Shortcomings hizi katika jeshi la polisi inabidi ziwe addressed kikamilifu kama kweli tuna nia ya kupambana kikamilifu na uhalifu wa aina hii.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...