MAKAMPUNI
ya kitalii hapa nchii yametakiwa kuutangaza kwa kiasi kikubwa utalii wa
vivutio vyetu hapa nchini ndani ya nchi pamoja na nje ya nchi ili
kuwapa wanachi moyo wa kizalendo katika kujali vivutio walivyo navyo.
Hayo
yalisemwa juzi jijini Arusha na waziri wa Maliasili na utalii Mh.
Lazaro Nyarandu wakati akifungua mkutano wa 30 wa asasi ya wamiliki wa
makampuni ya kusafirisha watalii TATO ambapo alisema kuwa hii ndio
nafasi kubwa waliyokuwa nayo makampuni hayo makubwa ya uendeshaji
shughuli za kitalii.
Pamoja
na hayo pia ameyataka makampuni hayo ya kitalii kuhakikisha yanaongeza
kiasi kikubwa cha watalii wanaoingia hapa nchini ili kuingizia serekali
fedha nyingi za kigeni na kuachana na kasumba iliyozoeleka ya kupandisha
ada ya kiiingilio cha katika hifadhi zetu pamoj a na vivutio.
Aidha
kwa upande wa kutunza utalii wa Utamaduni Waziri wa maliasili mh.
lazaro Nyarandu amezitaka kampuni hizo zinazohusika na kuwa shafirisha
watalii katika mbuga kuhakisha wanawapitisha watalii katika sehemu za
kiutamaduni kwa maana kama wanyama watalii wameshawaona na upande wa
utamaduni nako kuna ulazima mkubwa sana.
Pia
Waziri wa maliasi na utalii alisema kuwa kwa sasa wizara yake
imejipanga katika kutangaza utalii hapa nchini na sasa hivi wanaanza
kutangaza katika shirika katika mashirika makubwa ya habari kiwemo
Shirika la hababri la BBc pamoja na CCN.
Naye
Mwenyekiti wa TATO Bw. Willey Chambulo ametoa malalamiko yake kwa
serekali na kuwakilisha kwa waziri wa Maliasili Mh. Lazaro Nyarandu
kuhusiana na tatizo la hivi karibuni la kuwepo kwa mageti yasiyo rasmi
katika baadhi ya hifadhi hapa nchini.
Alisema
kuwa, hii imetoke hivi karibuni katika mbuga ianayomilikiwa na TANAPA
mnamo tarehe 01 mwezi huu na kudaiwa ongozeko la kodi amabalo wao
hawakuwa taarifa na hivyo kuwapa usumbufu kupelekewa kukamatwa kwa
watalii waliokuwepo kuzuiliwa na kuwekwa chini ya Ulinzi hivyo kupelekea
kurudisha nyuma hali ya utalii hapa nchini.
Hata
hivyo Waziri wa Maliasili Mh. lazaro Nyalandu alijibu malalamiko hayo
kwa kusema kuwa akiwa kama waziri mwenye dhamana ameshatoa maagizo kwa
mamlaka zote za uhifadhi pamoja na mbuga kusitisha mara moja kusumbua
watalii na kuwataka kutumia lugha nzuri katika kudai mapato.
Mkutano
huu wa TATO wa 30 unatarajiwa kupitia Mahesabu yaliyopita pamoja na
kufanya uchaguzi wa kuchagua viongozi wapya wa Asasi hiyo.(Pamela Mollel wa jamiiblog).
Ankal, katika kublogu kwa miaka kadhaa, nimethibitisha kuwa blogu ina nafasi katika kutangaza utalii. Makala mbili tatu nilizoandika katika blogu yangu ya ki-Ingereza, kuhusu Mbambabay, Lushoto, na hasa moja iitwayo ""Tourism in Longido," zinatembelewa sana na wadau kutoka sehemu mbali mbali duniani.
ReplyDeleteMfano hai: Wajerumani fulani waliniandikia, kutokana na waliyosoma kwenye blogu yangu kuhusu Mbambabay, nikawa mshauri wao katika kupanga safari ya Mbambabay. Walisafiri.
Kwa hivi, pamoja na kutambua na kupongeza mchango wa makampuni ya utalii katika kutangaza vivutio, hata blogu inaweza kutoa mchango fulani, katika huu utandawazi na teknohama.