Katika kuendelea kusherehekea Muungano wetu na pia
kujiunga na wenzetu wa nchi ya Zambia ambao nao mwaka huu wanasherehekea miaka
50 tangu wapate Uhuru (25 Oktoba), Ubalozi wa Tanzania nchini Zambia unapenda
kuwajulisha kuwa umeandaa maonesho ya bidhaa zinazozalishwa nchini Tanzania.
Ubalozi wa Tanzania nchini Zambia unachukua nafasi hii
kuwakaribisha rasmi Watanzania kuja kushiriki katika maonesho haya. Tuna amini
ni nafasi nzuri ya kujitanganza na kuonana uso kwa uso na wadau mbalimbali ili
kupanua wigo wa biashara.
Maonesho haya ambayo yamebeba jina la "TANZANIA
WEEK" yatafanyika katika viwanja vya Ofisi ya Ubalozi Lusaka, Zambia,
kuanzia tarehe 25 hadi 31 Julai 2014. Nafasi bado ipo.
Nukushi ya Ubalozi: tanzanhighcom@zambia.co.zm
Namba ya Simu: +260211253323/4
Maafisa
wa Ubalozi;
i) Bibi Justa M. Nyange - simu ya kiganjani
+260-979-401-433
Nukushi : kitutuj@yahoo.com
ii) Bw.
Richard M. Lupembe - simu ya kiganjani
+260-965-031-754
iii) Bw.
Mogosi S. Munatta - simu ya kiganjani +260-979-411-011
iv) Bw.
Huddy A. Kiangi …….simu ya kiganjani +260-977-934-240
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...