Aisha Sururu Foundation inawataarifu fainali ya mashindano ya kuhifadhi Qur'an Tukufu ya kitaifa ya mwaka 2014 yatafanyika Jumapili hii ya tarehe 13/07/2014 katika ukumbi wa Diamond Jubilee Hall ambapo vijana wanawake na waume walioshiriki katika mashindano hayo watapigania nafasi zao za kwanza mbele ya umma na wageni waalikwa katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhan.
Mwaka huu Aisha Sururu Foundation imeshirikisha mikoa 9 ya Tanzania ikiwemo visiwa vya Zanzibar na Pemba ambapo vijana watakaoshiriki kutoka visiwa vya Pemba ni vijana walemavu wa macho, walemavu wa viungo na kadhalika. Njoo uje ushuhudie uwezo wa Allah (Mwenyezi Mungu) vipi walemavu wa macho na vijana wengineo walivyojiwezesha kufika kwenye jukwaa la mashindano ya kuhifadhi Qur'an ya kitaifa ya mwaka 2014.
Uongozi wa Aisha Sururu Foundation unawaalika Watanzania wote waje pamoja kushuhudia mashindano haya na kuwashajiisha vijana wote walioshiriki katika mashindano haya ya kitaifa ya mwaka 2014.
Ukumbi wa Diamond Jubilee Hall, Tarehe 13/07/2014, Jumapili
Kuanzia saa tatu asubuhi (9am) mpaka saa nane mchana (2pm)
Wabillahi Tawfeeq,
Ramadhan Mubaarak,
Allah awalipe
ReplyDeleteMashallah.
ReplyDeleteKuhifadhi? Silewi naomba mnieleweshe asante.
ReplyDeleteKuhifadhi ni kusoma aya zilizomo ndani ya Qur'an bila ya kutizama kitabu chenyewe, kwa kuwa umehifadhi kwa moyo wako. Shukran.
ReplyDeleteAu kwa kizungu ni cram
ReplyDeleteor to memorize