Na John Nditi, Morogoro
Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makalla ,ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji,kuanzia Julai 3 hadi 7, mwaka huu, alifanya ziara ya kikazi iliyilenga kuhamasisha shughuli za maendeleo ya wananchi wake wa vijiji mbalimbali vya Tarafa ya Mlali, Turiani na Mvomero.
Katika ziara hiyo, ametoa misaada ya aina mbalimbali ya kifedha na vifaa kwa ajili ya kuharakisha maendeleo ya huduma za kijamii ikiwa ni pamoja na kuzundua vituo vya kuchota maji Kijiji cha Mgogo, Kata ya Sungaji, Kijiji cha Mlali na Kipera, kutoa misaada ya kifedha kwa vikundi vya akina mama wajasiliamali, vijana , taasisi za dini na ujenzi wa ofisi za CCM kata na Matawi.
Sehemu kubwa ya misaada ya kifedha ilielekezwa kwenye sekta ya elimu katika kusaidia uendelezaji wa ujenzi majengo ya madarasa la shule za awali na mikondo ya darasa la kwanza kwenye vijiji vilivyopo kwenye Tarafa hizo kufuatia wananchi kuonesha nguvu zao wakiwa na lengo la kuwaondolea adha watoto wao wanaotembela umbali mrefu kwenda shule.
Mbunge hiyo pia akiwa Mji Mdogo wa Dakawa, alikabidhi msaada wa vyakula kwa kutoa tende katoni 50 na mchele tani 1.5 kwa ajili ya waumini wa dini ya kiislamu ambao wapo kwenye mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan wilaya huo.
Baadhi ya wanawake wa vikundi vya vicoba wakimsikiliza mbunge wao (hayupo pichani) kwenye mkutano wa hadhara eneo la Dakawa.
Kazi imeenda vizuri,msimamizi wa mradi maji akimnong'oneza Naibu Waziri wa Maji ambaye ni Mbunge wa Mvomero, Amos Makalla (mwenye shati la kitenge).
Kuwafikia wananchi wa kutumia njia ya miguu sehemu ambako hakuna daraja la kupita magari.
Mbunge Amos Makalla ambaye ni Naibu Waziri wa Maji, akimtwisha mmoja wa wakazi wa Kijiji cha Mlali ndoo ya maji baada ya kuzindua kituo cha kuchota maji.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...