1
Mbunge wa Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete na Diwania wa Kata ya Bwilingu Bw. Ahmed Nasser wakiwa wamelala kwenye moja ya vitanda Vitanda 267 vilivyotolewa na mbunge huyo katika shule mbalimbali za sekondari kwa jimbo zima la Chalinze wakati wa makabidhiano yaliyofanyika kwenye shule ya sekondari ya Lugoba jana, Shule ambazo zimepewa vitanda hivyo ni shule ya sekondari Chalinze 50, Moleto Lugoba 50, Mandera 25, Talawanda 24, Kiwangwa 50, Lugoba 38 na Kikaro 30.katika hatua hiyo Mh. Ridhiwania pia amepiga hatua kwa kutekeleza mambo mbalimbali aliyoahidi wakati wa kampeni zake. Katika utekelezaji huo ametoa Baiskeli 10 kwa walemavu, Miwani na mafuta kwa Maalbino, Jezi pea 100 kwa ajili ya mbunge Cup mashindano ambayo yataanza baada ya mwezi mtukufu wa Ramadhan, Visima 3 kata ya Kibindu, na 16 kwa shule zote za sekondari jimbo zima kila shule kisima kimoja kitachimbwa.
Ametoa Transforma kubwa ya umeme kata ya Lugoba na kumaliza kabisa tatizo la umeme katika kata hiyo, Kwa upande wa barabara amesema mvua zimekwisha hivyo barabara zote za jimbo hilo ambazo ziliharibwa na kutopitika sasa zitafunguliwa baada ya kupatikana kwa mdau ambaye atatoa mashine (Mitambo)za kukarabati barabara na mafuta yapo ya kutosha kuhakikisha kazi hiyo inakamilika kabla ya kuanza tena kwa mvua za masika ili kuzinfungua upya.
Mh. Ridhiwani pia ametoa mipira kwa shule za Msingi jimboni humo,, ametoa Microscope kwa Zahanati ya kanisa Lugoba. na atajenga darasa 1 shule ya msingi Kiwangwa.
Wengine katika picha kulia ni Abukbakary Mlawa Meneja Uhusiano wa kampuni ya Mamba Cement ambayo ndiyo iliyotoa vitanda hivyo na kushoto ni Diwani wa Kata ya Lugoba Bi Rehema Mwene.
3
Mbunge wa Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete na Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Mamba ment ambayo ndiyo iliyotoa vitanda hivyo wakivikabidhi kwa Diwani wa kata ya Bwilingu Bw. Ahmde Nasser na Mwalimu Mkuu wa Shule ya sekondari Chalinze Bw. Emmanuel Kahabi katika makabidhiano yaliyofanyika kwenye shule ya sekondari ya Lugoba.
4
Mbunge wa Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete akimkabidhi vitanda Mkuu wa shule ya seondari ya Sekondari ya Mandera Bi. Rose Jumila, kushoto ni Diwania wa Viti maalum kata ya Msoga Bi. Maria raban Moreto.
5
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya Lugoba wakipiga pichya pamoja mbele ya vitanda hivyo kwa niaba ya wenzao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 07, 2014

    Safi sana hii muda wa maneno umekwisha sasa ni vtendo, hongera kamanda

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...