Mbunge wa Viti maalum(CCM) mkoa wa Arusha
Namelok Sokoine akiangalia bweni la shule hiyo ya Irkisongo wilayani Monduli
lililoteketezwa na moto
Mapacha wanaoishi Wakaazi wa New York Marekani
Joy na Jane wakimkabidhi mkuu wa shule hiyo mama Nyange sehemu ya msaada wao wa
kilo zaidi ya kumi za misumari
Mjumbe wa kamati ya siasa(CCM) wilaya Monduli,
Paulina Ngoyai(Mama Kalaine) akikabidhi msaada wake wa mifuko mitano ya sementi
kwa shule hiyo
Mbunge wa Viti maalum mkoa wa Arusha(CCM)
Namelok Sokoine akimkabidhi mwalimu mkuu wa shule ya sekondari Irkisongo
wilayani Monduli Happiness Nyange msaada wake wa shilingi millioni moja
kufuatia kuungua kwa mabweni ya shule hiyo
![]() |
Mwakilishi wa kiwanda chaTanfoam cha jijini Arusha Sajid Ibrahim(kulia)
akimkabidhi sehemu ya msaada wa magodoro 100 yenye thamani ya shilingi millioni
3 kwa mwalimu mkuu wa shule ya sekondari ya Irkisongo Wilayani Monduli Happness
Nyange(kushoto), kufuatia mabweni ya shule hiyo kuteketea kwa moto hapo
jana.Msaada huo unatokana na harambee ya papo kwa papo aliyoifanya mbunge wa
Monduli Mh Edward Lowassa akitumia simu yake ya kiganjani. Wadau kadhaa wa
elimu wamejitokeza kusaidia ambapo mbunge wa Arusha Viti maalum Namelok Sokoine
amechangia shilingi millioni moja.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...