Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi mwishoni mwa wiki (Julai 3) alifanya ziara ya kutembelea zahanati ya kijiji cha Mkonze Manispaa ya Dodoma kukagua kazi ya ukarabati wa Jengo la Zahanati ya kijiji hiko lililokuwa limetokewa na nyufa kwenye baadhi ya kuta na kusababisha jengo hilo mali ya serikali lisitumike kutoa huduma kwa wananchi kwa sababu za kiusalama. 
 Kwa sasa jEngo hilo linaendelea kufanyiwa ukarabati ikiwa ni kulijengea nguzo za zege kwenye kuta ili kuliongezea uimara na kuziba nyufa kwenye baadhi ya kuta za jengo hilo. 
Dr. Nchimbi alisisitiza mafundi na wasimamizi wa ukarabati huo kuweka nguzo za kutosha ili jengo lizidi kuwa imara. Katika hatua hii, Dr. Nchimbi amemuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma kuhakikisha anafanya mradi huo wa zahanati kuwa kipaumbele cha Manispaa ya Dodoma na kuhakikisha ukarabati wa jengo hilo unakamilika mara moja ili lianze kutoa huduma kwa wananchi na tayari ameshamuagiza Mhandisi ujenzi wa Mkoa wa Dodoma kwenda kwenye mradi huo kufanya Tathimini ya Kitaalamu ili kuweza kushauri ipasavyo. 
 Mradi huo unaonesha kulikuwa na hali ya kulega kwenye utekelezaji na usimamizi wa ujenzi wa jengo hilo na kuwa pamoja na ardhi ya eneo hilo kuwa na asili ya kuchanika na kuchangia nyufa kutokea lakini Mkuu huyo wa Mkoa amesema wataalamu hawakufanya kazi yao kitaalamu ndio maana kumejitokeza athari kama hizo . 
 Kwa upande wao wananchi wa Kijiji hiko wamelaumu kuwepo kwa tatizo la usimamizi hafifu wakati wa utekelezaji wa mradi huo na ndio maana changamoto hizo zimejitokeza. 
Akiwakilisha hoja za wananchi walio wengi mkazi wa kijiji hiko Ndg. Yusufu Yacob amemueleza Mkuu wa Mkoankuhakikisha ukarabati huo unasimamiwa kwa karibu ili kutibu dosari zilizopo kwenye jengo hilo ili lianze kutoa huduma na wananchi waanze kunufaika na mradi huo wa Afya kwani kwa sasa wanalazimika kuzifuata huduma hizo mjini Dodoma kwa umbali mrefu jambo ambalo ni adha kubwa kwao. 
 Ikumbukwe kuwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliwahi kutembelea Mradi huo mapema mwezi Machi na kujionea dosari hizo kwenye jengo hilo na kumuagiza Mkurugenzi wa Manispaa Dodoma na Timu yake ya Watendaji kulifanyia haraka ukarabati jengo hilo lianze kutoa huduma lakini aliporudi Mwezi Juni kuangalia utekelezaji wa maelekezo yake alikuta hali isiyoridhisha.
 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi akikagua nguzo zilizojengwa kwa lengo la kuongeza uimara kwenye jengo la zahanati ya kijiji cha Mkonze Manispaa ya Dodoma lililokuwa limeathiriwa na nyufa kwenye baadhi ya kuta na kusababisha rasilimali hiyo ya serikali isitumike kutoa huduma kwa wananchi kwa sababu za kiusalama, Mkuu huyo wa Mkoa alifanya ziara hiyo
 Jengo la zahanati ya kijiji cha Mkonze Manispaa ya Dodoma likiwa limeanza kujengewa nguzo kwenye kuta kwa lengo la kuliongezea uimara, Jengo hilo lililokuwa limeathiriwa na nyufa kwenye baadhi ya kuta na kusababisha rasilimali hiyo ya serikali isitumike kutoa huduma kwa wananchi kwa sababu za kiusalama.
 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi (katikati) akizungumza na baadhi ya Viongozi wa kijiji cha Mkonze, wajumbe wa kamati ya Afya kijijini hapo na baadhi ya watumishi wa Manispaa ya Dodoma mapema jana Julai 3 wakati alipotembelea zahanati ya Kijij hiko kukagua ukarabati wa jengo la zahanati ya kijiji lililokuwa limeathiriwa na nyufa kwenye baadhi ya kuta na kusababisha rasilimali hiyo ya serikali isitumike kutoa huduma kwa wananchi kwa sababu za kiusalama.
Jengo la zahanati ya kijiji cha Mkonze Manispaa ya Dodoma ambalo lilikuwa limeathiriwa na nyufa kwenye baadhi ya kuta na kusababisha rasilimali hiyo ya serikali isitumike kutoa huduma kwa wananchi kwa sababu za kiusalama kwa sasa linafanyiwa ukarabati kwa kuanzia na kujengewa nguzo ili kulipa uimara na kuondoa mapungufu yaliyojitokeza ili jengo hilo lianze kutoa huduma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...