Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akizungumza kwa hisia kubwa na wanafunzi wa shule ya Sekondari Itwelele iliyopo Manispaa ya Sumbawanga leo tarehe 15/07/2014 ikiwa ni siku ya pili ya ziara yake ya kuhamasisha mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) kwa shule za Msingi na Sekondari Mkoani Rukwa. Katika ziara yake hii amepata fursa ya kuonana na wanafunzi na wadau wa elimu zikiwemo kamati za shule mbalimbali katika kata za Manispaa ya Sumbawanga na viongozi katika kujadili na kuweka mkakati wa kufanikisha mpango huo. Katika kuhakikisha BRN inafanikiwa ametoa maagizo kadhaa kwa viongozi husika ikiwemo kila shule ya msingi kuhakikisha kuwa na darasa la awali, kila shule ya sekondari kuwa na maabara ya sayansi, kila shule kutengeneza matofali 150, 000 na kila mzazi au mwananchi wa kata husika kutoa mchango wa Tsh. 10,000/= kusaidia ujenzi wa maabara hizo na madarasa.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya (kushoto) akizungumza na viongozi wa Manispaa ya Sumbawanga wakati akikagua moja ya maabara iliyokwishajengwa katika shule ya Sekondari Itwelele.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya (kulia) akizungumza na wananchi wa kata ya Pito wakiwa katika zoezi la kufyatua matofali kwa ajili ya ujenzi wa madarasa na maabara katika shule za kata hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akikagua sehemu ya mahindi yaliyozalishwa katika shamba la shule ya Sekondari Itwelele ikiwa ni matunda ya mpango ulioanzishwa na Serikali ya Mkoa wa Rukwa wa kugawa ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa shule zote Mkoani Rukwa ambazo zilitakiwa kulima shamba lisilopungua ekari tano litakalotumika kama shamba darasa na kusaidia upatikanaji wa chakula kwa shule husika. 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akizungumza na wadau wa elimu katika kata za Katandala, Izia na Majengo jana tarehe 14/07/2014 katika shule ya Sekondari Mazwi mjini Sumbawanga. 
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Sumbawanga akifafanua moja ya jambo katika kikao hicho. Alieleza kuwa kero inayowakabili wananchi na wanafunzi wa shule iliyokaribu na Dampo la Jangwani inakaribia kuisha kutokana na ujio wa magari mawili mapya ya kubebea taka yanayotegemewa kuwasili wiki hii mjini Sumbawanga.
Baadhi ya wadau wa elimu kutoka kata za Katandala, Izia na Majengo Mjini Sumbawanga wakiwa katika kikao cha kujadili mkakati wa kufanikisha mpango wa Matokeo Makubwa sasa (Big Result Now) kilichoitishwa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya (hayuko pichani).- Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @rukwareview.blogspot.com.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...