Baadhi ya Wanamuziki wa Bendi ya Msondo Ngoma 

 Magwiji wa muziki wa dansi nchini, Msondo Ngoma Music Band ‘Mambo Hadharani’ na Mlimani Park Orchestra “Sikinde Ngoma Ya Ukae” kesho mchana watachuana vikali katika viwanja vya TCC Club  Chang’ombe, Temeke.

Mpambano huo wa Nani Mtani Jembe ni kwa ajili ya kusherehekea sikukuu ya Idd el Fitri na pia litaamua ni bendi ipi kali kati yao.

Mratibu wa mchuano huo, Joseph Kapinga amesema pambano hilo litaanza saa nane alasiri hadi majogoo.

Kapinga alisema bendi zote mbili ziliwasili jana kutoka msituni walipojificha kujiandaa na mpambano huo.

Mratibu huyo alisema kila bendi itapiga kwenye jukwaa lake ili kulinda upinzani wao.
Katika pambano hilo, Msondo ndiyo watakaoanza kupanda jukwaani na baadaye Sikinde watakuwa wakijibu mashambulizi.
Baadhi ya wanamuziki wa Sikinde.

Kiongozi wa Msondo Ngoma Saidi Mabera  alisema jana watapiga nyimbo zao zote kali ili kuhakikisha wanaisambaratisha Sikinde.

Baadhi ya wanamuziki wanaounda Msondo Ngoma ni Shaaban Dede, Mabera,  Eddo Sanga, Juma Katundu, Roman Mng’ande `Romario’  na Hassan Moshi.

Naye kiongozi wa Sikinde Hamisi Mirambo alijigamba kuwa wataibuka na ushindi mnono.
“Tuna waimbaji wazuri na hakuna itakachotuzuia kushinda,” alisema Mirambo.

Baadhi ya wanamuziki wanaounda Sikinde ni Hassan Rehani Bitchuka, Hassan Kunyata, Abdala Hemba, Musemba Waminyugu.

Ramadhani Mapesa, Adofth Mbinga, Kelvin Mausi Mjusi Shemboza, Tonny Karama, Bonny Bass, Habibu Abass Jeff , Juma, Juma Choka, Mbaraka Othman, Hamisi Mirambo, Ali Yahaya, Yusuph Benard na Ali Jamwaka.

Pambano imeandaliwa na Keen Arts na Bob Entertainment chini ya udhamini  wa Konyagi na Saluti5.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...