WILAYA ya Mkuranga katika mkoa wa Pwani imepanga kupeleka Mwenge wa uhuru katika kijiji cha wasanii kilichopo MWANZEGA, Mkuranga Julai 22, mwaka huu, Mwenyekiti wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA), Cassim  Taalib amesema 


Bw. Taalib kasema kuwa mwenge utapokelewa kutoka wilaya ya Rufiji katikia kijiji cha Kiparang’anda na baadaye utakwenda moja kwa moja katika kijiji cha wasanii na wanamichezo cha Mwanzega ambako utawasili saa 7 mchana.

Alisema kutokana na ujio wa ugeni huo mkubwa SHIWATA imetangaza ofa ya  siku kumi ambapo itapokea wanachama kwa punguzo la asilimia 50 na kugawa bure viwanja vya kujenga nyumba wasanii na wanamichezo ambao watapata nafasi ya kwenda katika sherehe na watakabidhiwa viwanja vyao.

Wasanii na wanamichezo zaidi ya 600 wanatarajiwa kuondoka makao makuu ya shiwata ilala bungoni saa 12 asubuhi Jumanne asubuhi kwenda mkuranga.
Katika sherehe hizo kiongozi wa mbio za Mwenge, ataweka jiwe la msingi katika kijiji cha wasanii kuzindua rasmi kijiji hicho ambacho kinatarajiwa kuwekwa umeme, barabara na miundombinu ya kisasa.

Taalib alisema katika sherehe hizo msanii  maarufu wa atavishwa joho ya kutawazwa kuwa balozi wa kwanza wa kijiji cha wasanii na wanamichezo hapa nchini, na kuongezea kuwa  "SHIWATA pia inatoa pongezi kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mkuuu wa Wilaya ya Mkuranga, Viongozi wa Tarafa ya Shungubweni kata ya Mbezi,viongozi wa Mwanzega,Ngarambe. Alisema kutakuwa na mkutano wa wasanii

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...