Waimbaji nyota wa muzki wa Injili,Anastazia Mukabwa akiwa amepozi na Rose Muhando.
MWIMBAJI nguli wa muziki wa Injili nchini Kenya, Anastazia Mukabwa, ni miongoni mwa wakali ambao mwimbaji Rose Muhando anatamani wawepo kwenye uzinduzi wa albamu yake ya Kamata Pindo la Yesu.
Rose Muhando amepanga kuzindua
albamu yake ya Kamata Pindo la Yesu Agosti 3, mwaka huu ukumbi wa Diamond
Jubilee Dar es Salaam.
Akizungumza na gazeti hili, Muhando
alisema Mukabwa aliyemshirikisha katika wimbo wa Vua Kiatu ni aina ya wasanii
wenye uwezo mkubwa wa kuimba na kwamba tayari ameiomba Kamati ya Maandalizi ya
uzinduzi wake iwasiliane na msanii huyo kuhakikisha anapatikana siku hiyo.
“Wapo waimbaji wengi wa Injili
natamani wawepo siku hiyo, lakini ningefurahi kama ningempata Anastazia Mukabwa
wa Kenya, hivyo tayari nimeiomba Kamati ya Maandalizi ifanye kila iwezalo aje.
“Ni aina ya uzinduzi wa pekee ambao
nataka ufanyike siku hiyo, ni imani yangu tutampata Mukabwa na wakali wengine,”
alisema na kuongeza kuwa ujio wa Mukabwa utakuwa mzuri ili mashabiki 'wavue
viatu' siku hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...