Naibu Waziri wa Wizara ya
Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba (kulia), akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya
Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Mr. Salim Msoma wakati alipotembelea shirika
hilo mwishoni mwa wiki kuongea na Bodi, Menejiment na wafanyakazi wa Shirika
hilo. Nyuma ya Mr Msoma ni Kaimu Mtendaji Mkuu wa Shirika hilo, Kapteni Milton
Lazaro.
Naibu Waziri wa Wizara ya
Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba akisisitiza jambo wakati wa kikao chake na wajumbe
wa bodi na menejiment ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), wakati alipoongea
nao mwishoni mwa wiki katika ofisi za Makao ya Shirika hilo.
Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk.
Charles Tizeba, akisisitiza jambo wakati alipoongea na Bodi, Menejimenti na
wafanyakazi wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Naibu Waziri aliwasisitiza
watumishi hao kufanya kazi kwa bidii na kurudisha sifa ya shirika hilo. Picha na kitengo cha Mawasiliano
Serikalini-Uchukuzi
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...