Naibu
Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba, akifafanua jambo wakati
akiongea na Menejimenti na wafanyakazi wa Wakala wa Ndege za Serikali Tanzania (Tgfa),
alipokutana nao hivi karibuni. Naibu Waziri Tizeba aliwapongeza wafanyakazi hao
kwa kazi nzuri wanayoifanya kwa kuwahudumia vyema Viongozi mbalimbali wa
Kitaifa.
Mkurugenzi
wa Idara ya Uhandisi katika Wakala wa Ndege za Serikali Tanzania (TGFA),
Mhandisi Julius Shaba, akieleza jambo katika hanga ya Wakala huo kwa Naibu
Waziri wa Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba (wa pili kutoka kwa kulia), wakati
alipotembelea ofisi za Wakala huo na kuongea na wafanyakazi hivi karibuni.
Kulia wa Waziri Tizeba ni Mkurugenzi Mkuu wa Wakala huo Kapteni Kenan Mhaiki.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...