Kwa mujibu wa taarifa hiyo imedaiwa kuwa Sheikh huyo amejeruhiwa sehemu
mbalimbali ikiwemo miguu yake yote miwili sehemu za mapajani pamoja na Kifuani
na kupoteza baadhi ya vidole vya miguu yote miwili.
Mbali na Sheikh huyo pia kuna mtu mwingine aliyekuwa nyumbani kwake hapo
aliyetajwa kwa jina la Muhaji Kifea (38) ambaye ni mkazi wa Dar es salaam naye
amejeruhiwa na wote wamelazwa katika hospital ya mkoa Mount Meru kwa ajili ya
matibabu.
Akizungumza hospitalini hapo sheikh Sood amesema tukio hilo lilitokea
nyumbani kwake eneo la majengo ya chini ,usiku wa kuamkia leo majira ya saa 5
wakati yeye pamoja na mgeni wake walikuwa wakila chakula sebuleni Amesema alishangaa kusikia mlio mkubwa ulioambatana na vyuma mbalimbali
vilivyokuwa vikiruka hewani ,ambapo bomu hilo linaelezwa kuwa ni guruneti
lililorushwa kupitia dirishani baada ya watu wasiofahamika kufanikiwa kuvunja
kioo cha dirisha la chumbani katika nyumba hiyo.
Ameongeza kuwa wahusika wanafahamika maana walishawahi kumtishia kupitia
waraka wa maandishi pamoja na kumfyatulia risasi.
Amesema kuwa siku tatu kabla ta tukio hilo alikoswakoswa kwa
kupigwa risasi na watu wasiofahamika wakati akitoka msikitini na kutoa taarifa
katika kituo kikuu cha polisi jijiji hapa juu ya tukio hilo.
Sheikh Sood, ambaye ni kiongozi
Alswasun kanda ya kaskazini, inasemekana amekuwa akitofautiana na waamini wenzake kutokana
na msimamo wake mkali wa kutokukubaliana na makundi ya kigaidi yanayojiita
jihadi yanayotokana na vijana wenye msimamo mkali.
Inahofiwa waliofanya udhalimu wanahusika na vikundi vya ugaidi na
kwamba wanasakwa hivi sasa na vyombo vya ulinzi na usalama. Tutaendelea
kuwapasha taarifa zaidi kwa kadri zitavyopatikana.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...