Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Crescesius Magori (kulia) wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF akipata maelezo kutoka kwa Meneja Kiongozi, Uhusiano na Huduma kwa Wateja, Eunice Chiume (katikati) wa Shirika hilo alipotembelea banda hilo katika Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba). Wa pili kulia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano na Teknohama, Idi Khalfani, Kushoto ni Afisa Uhusiano Mwandamizi, Teopista Muheta.

Afisa wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii–NSSF
Mwadawa Asibawi akitoa maelekezo kuhusu
mikopo kupitia SACCOS inayotolewa na Shirika hilo kwa wanachama wake, Abdallah Majura. Katika mpango huo, wanachama wanaweza kufaidika na mikopo hiyo
ikiwa ni mpango wa serikali wa kuwawezesha wanachama wa mfuko huo kupambana na
umasikini.
Maafisa wa Shirika la Hifadhi ya jamii NSSF akisikiliza kwa umakini swali alilokuwa akiulizwa na mwanachama kuhusu mradi wa DEGE ECO VILLAGE katika maonyesho ya Sabasaba.Katika mradi huo wanachama wanaweza kununua nyumba za kisasa na nafuu. Kushoto ni Julius Nyamuhokya, Jumanne Mbepo(katikati) Na Aly Chwaya ( kulia)
Ofisa Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Christina Msengi akitoa maelezo kuhusu Mafao ya uzazi yatolewayo na Shirika hilo. Mafao haya hutolewa kwa wanachama wanawakee wanaotegemea kujifungua(wajawazito) au wameshajifungua.

Afisa Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Devotha Ikandilo (kulia), akizungumza na mwanachama kuhusu huduma mbalimbali
zitolewazo na shirika hilo. Kwa sasa wakulima na wachimba madini wadogo wadogo
wanaweza kujiunga na mfuko huu na kuweza kufaidika na mafao mbalimbali
yatolewayo na shirika hilo yakiwemo mafao ya matibabu, mafao ya kuumia kazini
na mafao ya uzeeni.
Afisa uhusiano wa
Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Said Mohamed akitoa maelezo kuhusu mafao
ya matibabu yatolewayo na Shirika hilo. Kwa sasa wafanyakazi na wale walio
katika sekta isiyo rasmi wanaweza kuchangia mfuko huo na kufaidika na mafao ya
matibabu yatolewayo na Shirika hilo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...