Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kufungua rasmi kituo cha afya katika Gereza la Kitai wilayani Mbinga jana.Kushoto ni Mkuu wa Gereza hilo Alexander Richard Nyefwe.Kituo hicho kitatoa huduma kwa askari magereza,wafungwa na vijiji jirani
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi miche bora ya kahawa mkulima mdogo Bi Dorothea Komba wakati alipolitembelea na kukagua shamba la kahawa AVIV Farm linalomilikiwa na kampuni ya Olam katika kijiji cha Lipokela wilayani Mbinga, mkoani Ruvuma leo.Kampuni ya Olam imepanga kutoa jumla ya miche milioni tatu kwa wakulima wadogo elfu mbili katika vijiji vinne vinavyozunguka shamba hilo katika kipindi cha miaka mitano ili kuwashirikisha kuzalisha kahawa bora.
 Meneja wa Shamba la Kahawa la AVIV Farm linalomilikiwa na kampuni ya Olam Bwana Medappa Ganapati akimuonesha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete mche bora wa kahawa iliyozaa vyema wakati Rais alipolitembelea na kukagua shamba la kahawa katika kijiji cha Lipokela, wilayani Mbinga Mkoani Ruvuma leo.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kufungua Soko la Kimataifa la Mkenda lililopo katika kijji cha Mkenda Mpakani mwa Msumbiji na Tanzania leo.kulia ni mbunge wa Peramiho Mh.Jenister Mhagama.Rais Kikwete yupo katika ziara ya kikazi Mkoani Ruvuma

 Sehemu ya  Soko la Kimataifa la Mkenda lililopo katika kijji cha Mkenda Mpakani mwa Msumbiji na Tanzania leo.Rais Kikwete yupo katika ziara ya kikazi Mkoani Ruvuma..(picha na Freddy Maro).


Saidieni watu kutoka kwenye umasikini, 
Rais awaagiza viongozi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amezitaka taasisi za Serikali kuongeza kasi ya kupunguza umasikini miongoni mwa wananchi, akisisitiza kuwa wananchi wamekaa katika umasikini kwa muda mrefu mno kupita kiasi.        
Rais Kikwete amesema kuwa wanachotarajia wananchi kutoka kwa taasisi za Serikali ni kusaidiwa kutoka kwenye umasikini kwa kasi kubwa zaidi kwa sababu wamekaa katika hali ya umasikini kwa muda wa kupita kiasi. 
Rais Kikwete ametoa maelekezo hayo leo, Jumapili, Julai 20, 2014, wakati alipokagua shamba la kisasa la zao la buni kwenye kijiji cha Lipokela, Wilaya ya Songea, ikiwa ni moja ya shughuli zake katika siku ya nne ya ziara yake ya siku sita katika Mkoa wa Ruvuma.
Rais Kikwete amesimama kwenye shamba hilo akiwa njiani kutoka Wilaya ya Mbinga kuelekea Wilaya ya Songea ambako leo amefungua soko la kimataifa katika kijiji cha Mkenda, kilicho mpakani kabisa mwa Tanzania na Mozambique. Baadaye, Rais amekagua daraja kwenye Mto wa Ruvuma ambalo linaunganisha Tanzania na Mozambique.
Rais Kikwete ametoa maelekezo hayo baada ya kuambiwa kuwa pamoja na kwamba shamba hilo, pengine ni kubwa kuliko jingine lolote la buni nchini, limefanikiwa kupata miche 3,000,000 ya buni za kisasa ambayo lilihitaji lakini wakulima wa kawaida wa zao hilo la kahawa wanashindwa kupatiwa kiasi hicho hicho cha miche ya buni.
“Kwanini tunashindwa kupata miche milioni tatu kwa ajili ya wananchi ambayo wenyewe mmesema kuwa gharama yake yak uizalisha ni shilingi milioni 900? Kwanini tunashindwa kupata miche ya kutosha ili wakulima wetu wapande na kuongeza kipatoc hao?”Rais Kikwete amemwuuliza Profesa James Teri, Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Utafiti ya Kahawa Tanzania (TACRI).
Ameongeza Rais Kikwete: “Hatuwezi kuwabakiza wananchi wetu katika umasikini kwa miaka mingine 30 kwa sababu tu hatuna uwezo wa kuzalisha miche ya kutosha. Hatuwezi kufanya hivyo, wameishi kiasi cha kutosha katika umasikini.”         
Amesisitiza Rais Kikwete: “Kazi yetu ni kuwatoa watu wengi zaidi katika umasikini kwa haraka kubwa zaidi kwa sababu wamechelewa mno. TACRI inaweza kufanya hivyo kwa kuwapa wananchi mbegu bora zaidi ya buni, ili waondokane na mibuni ya zamani ambayo uzalishaji wake ukochini. Hivyo, nataka kujua tunaweza kufanya nini kufanikisha hili siyo kuniambia habari ya changamoto ambazo TACRI inakumbana nazo katika kutimiza majukumu yake.”
Ameongeza Rais Kikwete: “Siridhiki na kasi ya kujaribu kuwatoa watu wetu katika umasikini. Nahitaji kupata miche milioni tatu kwa ajili ya wananchi wetu. Kama iliwezekana kulipatia shamba hilo miche milioni tatu kwa nini isiwezekane kwa wananchi?”
            Shamba hilo kubwa la mibuni (inayozalisha kahawa) ni mali ya Kampuni ya AVIV, ambayo ni kampuni tanzu ya Kampuni ya Olam International, ambayo inaendesha shughuli za biashara katika nchi 65 duniani.
Olam iliingia Tanzania miaka 20 iliyopita na shughuli zake kubwa ni katika mazao ya korosho na kiwanda cha kuchambua pamba kilicho Bunda, Mara.
Duniani, Olam ina mashamba ya mibuni katika nchi tano ambazo ni Tanzania, Zambia, Ethiopia, Laos na Brazil.
AVIV ambayo inapanda mibuni ya kuzalisha kahawa yaa ina ya Arabica ilipanda miche ya kwanza miaka mitatu iliyopita na inakaribia kuvuna kwa mara ya kwanza. Katika kijiji hicho cha Lipokela, AVIV ina ardhi yenye ukubwa wa hekta 2,000.Rais Kikwete anaendelea na ziara yake katikaMkoa wa Ruvuma leo kwa kutembelea na kukagua shughuli za maendeleo katika Wilaya ya Namtumbo.

Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
20 Julai,2014


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...