Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na wasanii nyota wa filamu na muziki kutoka Marekani walioko nchini kwa ziara ya kutoa mafunzo kwa wasanii wa Tanzania. Wasanii hao ni na Terrence J. Jenkins, mwendeshaji wa kipindi cha muziki kwenye televisheni ya E! Entertainment (wa pili kulia) Chaka Zulu, Mtendaji wa Shughuli za Muziki kutoka Kampuni ya Disturbing The Peace Records (wa pili kushoto) na Davis Banner, mwigizaji, mwanamuziki, mtunzi na msimamizi wa shughuli za muziki ambaye amepata kushinda tuzo maarufu ya Grammy.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitumia simu yake ya mkononi kuwaonesha vivutio vya kitalii wasanii nyota wa muziki na filamu wa Kimarekani walioko nchini kwa ziara ya kutoa mafunzo kwa wasanii wa Tanzania. Wasanii hao ni Terrence J. (Jenkins), mwendeshaji wa kipindi cha muziki kwenye televisheni ya E! Entertainment, mwigizaji wa filamu na mtunzi wa vitabu na Revi Shelton, Mtendaji wa Shughuli za Muziki katika Kampuni ya Outlet Media Group. Wengine ni Chaka Zulu, Mtendaji wa Shughuli za Muziki kutoka Kampuni ya Disturbing The Peace Records na Davis Banner, mwigizaji, mwanamuziki, mtunzi na msimamizi wa shughuli za muziki ambaye amepata kushinda tuzo maarufu ya Grammy.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akibadilishana mawazo na wasanii nyota wa muziki na filamu kutoka Marekani walioko nchini kwa ziara ya kutoa mafunzo kwa wasanii wa Tanzania. Wasanii hao ni Terrence J. (Jenkins), mwendeshaji wa kipindi cha muziki kwenye televisheni ya E! Entertainment, mwigizaji wa filamu na mtunzi wa vitabu na Revi Shelton, Mtendaji wa Shughuli za Muziki katika Kampuni ya Outlet Media Group. Wengine ni Chaka Zulu, Mtendaji wa Shughuli za Muziki kutoka Kampuni ya Disturbing The Peace Records na Davis Banner, mwigizaji, mwanamuziki, mtunzi na msimamizi wa shughuli za muziki ambaye amepata kushinda tuzo maarufu ya Grammy.PICHA NA IKULU.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa kwenye picha ya pamoja na wasanii hao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. MH.DR JK KIKWETE AMEFANYA JAMBO KUBWA NA LA KIHISTORIA KATIKA KUIMARISHA TASNIA YA MUZIKI NA SANAA,PIA AMEITANGAZA NCHI YETU NA KUIWEKA JUU KATIKA TASNIA HIZI!.MH.RAIS HONGERA SANA KWA HILI NA MENGINE MENGI UNAYOYAFANYA KATIKA TAIFA LAKO TANZANIA!.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 15, 2014

    Najiuliza nchi hii baada rais kustaafu atatokea rais kama huyu watanzania mtamkumbuka kikwete .ana sifa kwanza yuko karibu sana na wananchi wake pili yuko tayari kumsaidia yoyote aliye na kipaji afikie malengo yake msiba wa mtu anayemjua hata awe maskini kiasi gani atakwenda sasa mnaombeza mtamkumbuka

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 16, 2014

    Hata mie namkumbuka Mwana FA alivyosema kule Dodoma, kuwa wasanii wachangamkie fursa hizi anazotoa JK. Atakuja raisi hapa anayependa uvuvi mkaishia kuulizana maboti na nyavu za kuvulia. Wasanii kuweni wamoja, mumlipe JK fadhila zake kwa kufanya la maana. Akiondoka huyu mtamlilia wallahi... ohoooo...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...