Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Mhe. Richard Stuart Mann, Balozi wa New Zealand hapa nchini mwenye makazi yake Afrika Kusini. Hafla hiyo fupi ilifanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 15 Julai, 2014.
Balozi Mann akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) mara baada ya Balozi huyo kuwasilisha Hati zake za Utambulisho kwa Mhe. Rais Kikwete, wakwanza kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Kazi maalum Mhe. Prof. Mark J. Mwandosya (Mb.)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Mhe. Richard Stuart Mann
Balozi Richard Stuart Mann akisaini Kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili Ikulu.
Balozi Mann akisikiliza Wimbo wa Taifa lake ukipigwa kwa heshima yake mara baada ya kuwasili Ikulu. Kulia ni Mkurugenzi na Mkuu wa Itifaki, Balozi Mohammed Juma Maharage na wakwanza kushoto ni Mnikulu, Bw. Shaaban Gurumo.Picha na Reginald Philip.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...