Enzi hizo Raizoni hii iliyotengenezwa na kiwanda cha Bora Shoes Barabara ya Pugu Road (sasa Nyerere Road) kilikuwa kinauzwa kwa bei ya shilingi 320. Ukamilifu wa utanashati wa vijana wengi wa enzi hizo ulikuwa haukamiliki kama patakosekana shati la ndege la kubana, buga na hii Raizoni. Wenye data zaidi uwanja wenu huu...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 18, 2014

    The mdudu,mm katika kumbukumbu yangu nakumba wakati nikiwa mdogo kule Moro kuna binti walipendana na jamaa mmoja lakini cha kushangaza yule jamaa alikataliwa na wazazi wa yule binti,,mshenga wa yule bwana akauliza kwani tatizo ni nini? Yule mshenga akapewa jibu lake palele pasipo kuweka kipolo jibu alilopewa ni hili hapa MBONA MTU WAKO CHINI HANA hakiyamungu watu wote walibaki midomo wazi nayule bwana kilichomponza zaidi alikua peku peku,,mjomba Michuzi nakuomba basi utuandikie kitabu na humo ndani ya kitabu uweke mambo kama hayo ya Raizoni,suruwali za mchele mchele,buga,viatu vya komfuu,la kuchumpa,chachacha,na vinginevyo kibao

    ReplyDelete
  2. Na kichwani 'Afro' la nguvu likichanuwa. Mbali ya shati la ndege la kubana, pia kulikukwa na yale mashati ya vitambaa vya mpira a.k.a. no smoking, yaliyokuwa yakishonwa 'slim fit' mengine yakiachiwa kuchanuwa huku mikononi. Enzi hizo mabuga/mapekos yalikuwa na stlye fulani ya kusukwa sehemu za kwenye mifuko khususan miwili ya mbele. Hapo mtu bukheri kwenda kucheza 'Kamanyola bila jasho' na "masantula ngoma ya mpwita'.....kwa kweli 'Old is Gold' Na kama vile haitoshi pia walikuwa na 'majendo' yao ( miondoko yao maalum ukishatinga viwalo hivyo}. Sometimes uvaaji ule huwa naufananisha na ule aliovaa 'Diamond Platnumz' katika ile nyimbo yake 'Nataka kulewa' kwa kweli kila rika na enzi zake...lol

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 18, 2014

    Shuka tubonge hiyo

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 18, 2014

    Shati nla ndege liitwalo Juliana, pia suruali ya bugaluu ndo viliendana-KIVAZI

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 18, 2014

    Hivi viatu vilikuwa haviharibiki kabisa ndiyo maana mwenye navyo kavitoa alipovificha. mitindo huenda na kurudi pengine hivi karibuni zinaweza kurudi. Lakini hakuna anayekudai kama bado una raizoni zivae..

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...