Mwenyekiti wa Kikundi
cha Waendesha pikipiki Likotwa Manispaa ya Lindi, Bw. Maulid Said Mohamed
(kushoto) akimkabidhi Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana, Bw. James
Kajugusi risala kuhusu kikundi
hicho hivi karibuni Mjini Lindi. Mkurugenzi huyo alitembelea
kikundi hicho ili kukagua jinsi kikundi hicho kinavyofanya kazi na jinsi
kinavyonufaika na umoja huo. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Manispaa ya Lindi, Bw.
Daniel Kanuse.(Picha
na: Concilia Niyibitanga).
======== ======= =======
Serikali
kukopesha vikundi 453 vya Vijana
Na:
Concilia Niyibitanga - Afisa Habari Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo
Serikali inatarajia
kukopesha vikundi vya uzalishaji mali vya vijana vipatavyo 453 katika mwaka wa
fedha 2014/15 kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana. Hayo yamesemwa hivi
karibuni na Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana, Bw. James Kajugusi
alipotembelea kikundi cha Vijana waendesha pikipiki cha Likotwa kilichopo
Halmashauri ya Manispaa ya Lindi.
Lengo la Serikali ni
kuhakikisha kuwa vijana wanajiajiri wenyewe na kuondokana na dhana ya kutegemea
kuajiriwa ikizingatiwa kuwa kila mwaka vijana wapatao milioni 1.2 huhitimu vyuo
vikuu lakini wanaopata ajira za kuajiriwa ni vijana 200 tu. Amesema Bw.
Kajugusi.
Mikopo inayotolewa
kwa vijana kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana ni njia ya kuwakomboa vijana
kwa kuwaongezea mitaji ya kuweza kufanya shughuli za ujasiri na ujasiriamali na
hatimaye kujiajiri na kuajiri vijana wenzao.
Bw. Kajugusi
amekipongeza Kikundi cha Waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda cha Likotwa
kwa juhudi na mafanikio waliofikia hadi sasa kutokana na kuunda kikundi hicho
chenye lengo la kuboresha maisha ya waendesha pikipiki hao.Aidha, amewataka
kuzingatia sheria za usalama barabarani, kuzingatia maadili mema ili
kuimarisha amani na mshikamao katika
sehemu wanazoishi na vile vile
kuhakikisha wanatimiza wajibu wao kama vijana wa kulipa kodi.
Halikadhalika,
amekitaka kikundi hicho kuwahamasisha vijana wenzao kushiriki katika shughuli
za Mbio za Mwenge wa Uhuru na kuwaeleza manufaa ya mbio hizo na kuwapuuza
wanobeza Mwenge kwani wanaoubeza ni watumwa kwani wanaibeza historia ya nchi yao.
Naye kwa upande wake
Mwenyekiti wa Kikundi hicho, Bw. Maulid Said Mohamed amesema kuwa kikundi kina wanachama 13 na
pikipiki 2 zinazomilikiwa na kikundi na
hadi sasa wameshapatiwa viwanja 6 na Uongozi wa Manispaa kwa ajili ya kufanya
shughuli za maendeleo ya Kikundi.
Bw. Mohamed amesema
kuwa mpaka sasa kikundi kimejiwekea akiba na lengo kuu ni kuanzisha SACCOS kwa
ajili ya kuwakopesha vijana kwa riba nafuu na hatimaye kutengeneza ajira kwa
vijana wengi zaidi.
Kikundi cha Waendesha
pikipiki Likotwa kina wanachama 13 na kilianzishwa kwa nia ya kusaidiana na
kujiinua kiuchumi na kina malengo ya kuanzisha SACCOS kwa ajili ya kukopesha
vijana mikopo yenye masharti nafuu.
MWISHO
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...