Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohamed Gharib Bilal (katikati),Sheikh Mkuu,Issa Shaaban Simba,Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh. Said Meck Sadick na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Sheikh Mussa Salum wakijumuika na Waumini wengine wa Dini ya Kiislam kwenye Swala ya Eid El Fitr iliyofanyika Kitaifa kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja,Jijini Dar es Salaam leo.Picha zote na Othman Michuzi.



Sehemu ya Waumini wa Dini ya Kiislam wakiwa kwenye Ibada ya Eid el Fitr katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo.

Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam,Sheikh Mussa Salum akitoa Khotuba katika Idada ya Swala ya Eid El Fitr iliyofanyika Kitaifa kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja,Jijini Dar es Salaam leo.
Mawaidha yakiendelea mara baada ya Swala ya Eid el Fitr.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohamed Gharib Bilal akitoa salamu za Eid el Fitr leo mara baada ya Swala iliyofanyika Kitaifa kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja,Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ulinzi,Dkt. Hussein Mwinyi (katikati) akijumuika pamoja na Waumini wenzake wa Kiislam katika Swala ya Eid El Fitr iliyofanyika Kitaifa kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja,Jijini Dar es Salaam leo.
Masha ALLAH
ReplyDelete