Wakati Taifa Stars inaingia kambini Tukuyu mkoani Mbeya kesho (Julai 9 mwaka huu), kocha Mart Nooij amesema kambi ya wiki mbili nchini Botswana imekisaidia kikosi chake kujiandaa kwa ajili ya mechi dhidi ya Msumbiji.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo (Julai 8 mwaka huu) kuhusu maandalizi ya timu hiyo, Nooij amesema timu yake inafanya mazoezi kwenye maeneo ya baridi kwa sababu za kitaalamu, hivyo kambi ya Tukuyu kama ilivyokuwa ya Botswana itawasaidia kwa mechi dhidi ya Msumbiji.
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itaondoka kwa ndege kwenda Mbeya ikiwa na kikosi cha wachezaji 25, na itarejea jijini Dar es Salaam siku tatu kabla ya mechi hiyo.
Wachezaji walioko kwenye msafara huo ni Aggrey Morris, Aishi Manula, Amri Kiemba, Benedictor Tinoko, Deogratius Munishi, Edward Charles, Emmanuel Namwando, Erasto Nyoni, Haruni Chanongo, Himid Mao, John Bocco na Jonas Mkude.
Wengine ni Joram Mgeveke, Kelvin Friday, Kelvin Yondani, Khamis Mcha, Mrisho Ngasa, Mwagane Yeya, Nadir Haroub, Oscar Joshua, Pato Ngonyani, Ramadhan Singano, Said Juma, Said Moradi, Shomari Kapombe, Simon Msuva,
Mechi ya kwanza ya raundi ya pili ya michuano ya kutafuta tiketi ya kucheza fainali za Afrika (AFCON) dhidi ya Msumbiji itafanyika Julai 20 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...