Mshambuliaji wa timu ya soka ya Tanzania, Taifa Stars, Mbwana Samatta akitafuta mbinu za kuwatoka wachezaji wa Msumbiji katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
 Mbwana Samatta akiwatoka mabeki wa timu ya taifa ya Msumbiji. 
Mshambuliaji nyota wa Taifa Stars, Mbwana Samatta akiwa katikati ya mabeki wa timu ya taifa ya Msumbiji. 


Mshambuliaji wa timu ya soka ya Tanzania, Taifa Stars, Thomas Ulimwengu akimtoka beki wa Msumbiji, Zainadine Junior katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, wa kuwania tiketi ya Fainali za Afrika zitakazofanyika nchini Morocco mwakani. Timu hizo zilitoka sare ya 2-2. 
 Thomas Ulimwengu  akichuana na beki wa Msumbiji, Josemar Machaisse.

 Huniwezi...Mshambuliaji wa Taifa Stars, Thomas Ulimwengu akimtoka beki wa Msumbiji, Zainadine Junior.
 Mshambuliaji wa Stars, Khamis Mcha akiwa katika harakati za kufunga goli.
 Golikipa wa Stars, Deogratius Munishi akishangilia balo la pili la 
Taifa Stars kwa kuonyesha fulana yake iliyokuwa ikisomeka 'Sisi ni Watoto wa Rais Kikwete'.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 20, 2014

    Maandalizi ya mwenzi mzima ya taifa staz yangeelekezwa kwa timu ya vijana na ili mpira wetu ukue kuwe na conection ya kuwaingiza vijana wetu katika academy za timu za ulaya bila hivo tunatwanga maji kwenye kinu

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 21, 2014

    Kwa mwendo huu ni bora zije hizi serikali tatu ili tutunge katiba yetu ya Tanganyika ili tujipange upya na hiki kitu kinachoitwa FOOTBALL..kwasasa hizi ndio faida za kuokoteza wachezaji wenye ndevu toka simba,yanga,azam,wakati jinchi la Tanzania ni kubwa na vipaji lukuki lakini cha ajabu hatujui kuviandaa mapema,,coz haingii akilini kila mwaka wachezaji wanatoka simba na yanga wakati hizi timu hata viwanja vya kisasa hawana sasa ndio nini nyumbani 2-2 yaani hii kuonyesha ndio tushatolewa wamepata 2 ugenini watashindwa vipi wakiwa nyumbani,,na huyu kiongozi mpya wa TFF kaingia kwa makeke lakini mpaka sasa ziiii hana jipya wala mikakati ya maana yupo yupo tu namuomba aje hapa Uingereza ajifunze kwajinsi watu walivyo wabunifu,,sijawahi hata kumsikia angalau aseme au kuwabana viongozi wote wenye timu za football kuhakikisha wanajenga viwanja vya kisasa la sivyo timu zao zitafutwa,,simba na yanga mimi ndio nazichukia toka moyoni mwangu hii mitimu ipo siku nyingi sn lakini hawana cha kujivunia cha maana,,wao uwaambie kusajiri michezaji migeni na isiyo na vipaji coz hao wachezaji nikama wakwetu tu wanaokotezwa mitaani huko kwao lakini hii miongozi yetu wala haistuki kabisa yaani ovyo kabisa

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 21, 2014

    mabeki wanne wa msumbiji wamemzunguka samatta maana yake kulikuwa na wachezaji wanne wa taifa stars wako open. samatta alifanya nini na mpira huo?

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 22, 2014

    Anao anao Samatta na watu eh eh wanashangilia hakuna team work kumsaidia Samatta atoe pass ya counter attack ni kama vile wenzie wamesusa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...