Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Peter Ngota akionesha tuzo ya ushindi katika sekta ya mawasiliano.
Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya TTCL wanaoshiriki Maonesho ya 38 ya
Biashara ya Kimataifa wakipiga picha ya pamoja na tuzo yao mara baada
ya kutwaa tuzo hiyo.




KAMPUNI ya Simu Tanzania, TTCL imeshinda tuzo katika kundi la kampuni
zinazotoa huduma za mawasiliano, kwenye Maonesho ya 38 ya Biashara ya
Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es
Salaam.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Iddi ndiye aliyemkabidhi tuzo hiyo, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Peter Ngota
katika uzinduzi rasmi wa Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa jijini
Dar es Salaam yanayoendelea Viwanja vya Mwalimu Nyerere.
Ushindi
wa TTCL unatokana na ubora wa huduma zinazotolewa na kampuni hiyo
katika upande wa mawasiliano ya simu na pia mawasiliano ya intaneti
"DATA". TTCL imesema ushindi huo umeipa hamasa ya kuendelea kubuni
bidhaa ambazo zitakuwa chachu ya ukuaji uchumi nchini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...