MWIMBAJI mahiri wa nyimbo za Injili, Upendo Nkone ni miongoni mwa wasanii watakaosindikiza uzinduzi wa albamu ya Rose Muhando.Muhando anatarajia kuzindua albamu hiyo Agosti 3, mwaka huu ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam na kuendelea katika mikoa mbalimbali nchini ukiwemo Mwanza Uwanja wa CCM Kirumba, Agosti 10.
 
 Akizungumza na gazeti hili,  Muhando alisema Nkone tayari amekubali kushiriki katika uzinduzi huo na ana matumaini litakuwa tamasha la aina yake.Nkone ametamba na albamu mbalimbali ikiwemo Mungu Baba, Hapa Nilipo, Zipo Faida na Uniongeze Yesu.

Nyimbo zilizopo katika albamu hiyo mpya ya Muhando ni Bwana Niongoze, Wewe Waweza, Usiniache, Nibariki, Muongo, Kwema, Kamata Pindo la Yesu na Facebook.

Hivi sasa Muhando anatamba na albamu yake ya Utamu wa Yesu yenye nyimbo saba, ambazo ni Utamu wa Yesu, Raha Tupu, Tamalaki, Ndivyo Ulivyo, Woga Wako, Imbeni na Kusifu na Achia.


Mbali na Utamu wa Yesu, Rose Muhando pia amewahi kutamba na albamu za Uwe Macho, Nyota ya Ajabu (Zawadi ya Krismasi) na Jipange Sawasawa, Kitimutimu, Mungu Anacheka, Wololo.Pia amepata kung’ara katika wimbo wa Vua Kiatu, alioshirikiana na Anastazia Mukabwa wa Kenya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...