Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Sadifa Juma akimvisha kofia ya ukamanda
Profesa Peter Msolla baada ya kuteuliwa kuwa Kamanda wa UVCCM wilaya ya
Kilolo sherehe zilizofanyika katika viwanja vya Kidabaga.
Mbunge wa jimbo la Kilolo,Profesa Peter Msola akila kiapo cha kuwa
kamanda wa UVccm mbele ya Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Sadifa Juma.
Mbunge wa jimbo la Kilolo,Prof Peter Msola akiwaapisha makamanda wa
vijana ccm katika wilaya ya Kilolo sherehezz ilizofanyika katika uwanja
wa Kidabaga.
Na Denis Mlowe,Kilolo
MWENYEKITI wa Umoja wa Vijana Chama
cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Sadifa
Juma Hamis ametoa rai kwa vijana
kuepuka kutumika katika kuvuruga amani na utulivu uliopo nchini Tanzania kwa
kutumika na baadhi ya vyama vya siasa na kuhatarisha amani ya Taifa.
Sadifa alitoa rai hiyo mwishoni mwa wiki katika viwanja
vya Kidabaga wakati akiwahutubia wananchi wa Kidabaga kata ya Bomalang’ombe wilayani
Kilolo wakati wa kusimikwa kwa mbunge wa jimbo la Kilolo Prof. Peter Msola kuwa
kamanda wa umoja wa vijana CCM wa wilaya ya hiyo.
Alisema kuwa amani
ambayo tunajivunia ipo siku
itatoweka na iwapo vyama
vya siasa vitaacha kufanya kazi
yake ya kisiasa kwa kunadi sera
za vyama vyao na kueneza chuki
dhidi ya serikali kama
ilivyo hivi sasa kwa baadhi ya vyama kuendesha siasa za
chuki na kuwatumia vijana
kuvuruga amani yetu.
" Nawaombeni
sana vijana wa kuendelea
kuonyesha mfano kwa vijana
bora katika kudumisha amani iliyopo na kamwe msije iga siasa vya
vyama vya upinzani siasa ya kufanya
vurugu ..... hiyo ni siasa mbaya
sana na itakuja kuliweka Taifa
katika umwagaji damu ambao hakika itakuwa ngumu sana kuweza kuishi tena kama
mwanzo” alisemaSadifa
Alitoa mfano kuwa kuna ushahidi kwa nchi jirani unaonesha
madhara ya kuichezea amani na kuongeza kuwa ni rahisi sana kupoteza amani na
umoja lakini ni vigumu sana kuirejesha na kuwataka vijana kuacha kuandamana kwa
kuiga tu kwa kuwa umeambiwa fanya jambo hilo
Mbali ya kuwataka
vijana kuacha kutumiwa na baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa Sadifa
aliwataka viongozi wa vyama vya siasa kutowatumia vijana hao katika kuvuruga amani pia aliwataka vijana
kutokubali siasa chafu zenye chembe ya
vurugu kwa watanzania na kuongeza kuwa sehemu yoyote yenye amani na utulivu,
yapo maendeleo kwa sababu wananchi wanafanya shughuli za maendeleo kwa uhuru
Kwa upande wake Kamanda mpya wa umoja wa vijana Ccm wilaya
ya Kilolo, Prof Peter Msola aliwataka vijana kufanya kazi kwa bidii kwa lengo
la kuondokana na umaskini katika wilaya hiyo na kuwataka kushirikiana katika
kudumisha amani iliyopo nchini Tanzania.
Alisema moja changamoto kubwa inayowakabili vijana na ambayo
kwa kushirikiana nao atahakikisha inafanyiwa kazi kwa kutumia fursa mbalimbali
zinazowazunguka ni ajira kwa kuwa fursa hizo zinaweza kuwa katika sekta ya biashara, kilimo na ushauri
kwa kupitia vikundi vya maendeleo.
Alisema ardhi na hali ya hewa nzuri ya wilaya ya Kilolo
inaweza kuwaongezea fursa ya ajira vijana wa wilaya hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...