Mbunge wa Jimbo la Kinondoni, Idd Azzan wa CCM (KULIA), akiamulia ugomvi wa Diwani wa Kimara, Pascal Manota wa Chadema (kushoto) na Mwenyekiti wa CCM, Wilaya ya Kinondoni, Salum Madenge waliotaka kuzichapa ulipotokea mzozo katika mkutano wa hadhara wa Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla katika Uwanja wa Shule ya Mavurunza, Kata ya Salanga, Jimbo la Ubungo, Dar es Salaam jana.
Wafuasi wa CCM na Chadema wakitaka kuzipiga kavu kavu baada ya kutokea mzozo ambapo wanaCCM walikuwa wakimzomea Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Mhe John Mnyika akihutubia na WanaChadema wakimzomea Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla akihutubia katika mkutano huo.
Polisi wakiwatuliza wafuasi wa Chadema waliokuwa wakipinga Mbunge wao John Mnyika asijibu swali lililoulizwa na Mkazi wa Kibamba, Jordan Balindo aliyemtaka Mnyika aeleze ni jitihada gani amezifanya binafsi kama mbunge kutatua changamoto ya ukosefu wa maji katika jimbo la Ubungo.
Naibu Waziri wa Maji, Mhe Amos Makalla (kushoto) na Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Mhe John Mnyika (Chadema), wakitofautiana jukwaani wakati Makalla akiamuru polisi kuwatoa wafuasi wa Chadema waliokuwa wakimzomea wakati akileleza Utakelezaji wa Ilani ya CCM JUU YA MAJI, HUKU mNYIKA AKITAKA WAENDEE KUZOMEA AKIDAI KWAMBA WAZIRI HAKUFANYA HAKI KWANI YEYE ALIPOKUWA AKIZOMEWA NA WANA CCM HAKUWACHUKULIA HATUA KAMA HIYO KATIKA MKUTANO WA HADHARA ULIOFANYIKA KATIKA UWANJA WA SHULE YA MAVURUNZA, KATA YA SALANGA. Picha zaidi BOFYA HAPA
Sasa haya mambo ya kuzitwanga vipi, vyama vilumbane kwa hoja siyo kwa ngumi.
ReplyDelete