Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba, Bw. Deus Kibamba akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo Julai 17, 2014 kuelezea msimamo wa JUKWAA LA KATIBA juu ya mwenendo uliopita wa bunge hilo. Picha na Cathert Kajuna wa Kajunason Blog

Kiongozi wa Shule Kuu ya Sheria nchini Kenya, Profesa Patrick Lumumba alisisitiza suala la wanasiasa kurudi bungeni na kuhakikisha katiba mpya inapatikana.

Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo.

Wajumbe wa JUKWAA LA KATIBA wakisisitiza jambo.
Na Hellen Kwavava, Dar es Salaam.
Ushauri Umetolewa kwa Wajumbe wa Bunge Maalum la katiba kuwa na Mtazamo mpya utakaoiletea nchi maslahi pindi watakaporudi bungeni katika mchakato wakutafuta katiba mpya unaotarajiwa kuanza mapema mwezi ujao.
Hata hivyo kundi la Umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA) limezidi kushauri wakirudi bungeni na kuendelea na majadiliano kwa msingi wa rasimu ya katiba.
Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam leo Julai 17, 2014 na mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba, Bw. Deus Kibamba ambapo ameeleza kwamba wabunge wanatakiwa kuachana na mtazamo wa kisiasa pamoja na lugha zisizo na staa kwenye bunge hilo kwani wanatakiwa kuzingatia uzalendo kwanza.
Aidha Bw. Kibamba amesema kwamba licha ya muda kuwa mfupi kuelekea katika uchaguzi wa mwaka 2015 wao wanapendekeza juhudi zaidi zifanyike ili kukamilisha upatikanaji wa katiba hiyo.
Naye Kiongozi wa shule kuu ya Sheria nchini Kenya Profesa Patrick Lumumba amewasihi wanasiasa wa nchini kuhakikisha katiba inapatikana kutokana na matakwa ya wananchi kwani nchini jirani zimekuwa zikiiga mambo mengi kutoka huku.
Bunge Maalum la katiba linatajiwa kuanza tena Agosti 5, 2014 mwaka huu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 18, 2014

    The mdudu,serikali 3 ni razima wala sio ombi mm huku nimegundua kitu nyeti toka kwa wazanzibar wanatuchukia sisi wa bara,hawatupendi kabisaa,wanasema wanataka nchi yao iwe huru,,sasa kwanini nasisi tusiwe na Tanganyika yetu? Dawa ya moto ni moto wala sio maji tena mtu akiwesha moto wa petrol na ww wesha wa gesi,,kwahiyo kukata mzizi wa fitina ni 3 tu.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 18, 2014

    Kikwete tuokoe; fukuza wote wale walitoka nje - UKAWA kwani uliwachagua!

    Nyerere aliwahi kufukuza Bunge; likarudi limeuficha mkia wake!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 18, 2014

    Katika kutoa mchango wao wajumbe wa Katiba wachhukulie dhamana waliyopewa na watanzania ya kutengeneza katiba kwa uzito unaostahili.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...