Wakaazi wa kata ya Mto wa Mbu waliwapongeza wafanyakazi hao kwa kujitolea na kuacha shughuli zao kwenda kuhimiza usafi wa mazingira ya mji wao huku wakiwataka wenzao kujali usafi wa mazingira ilikuepuka magonjwa ya milipuko
Kwa upande wake kaimu mhifadhi wa hifadhi ya ziwa manyara Ibrahimu Yamola alisema kuwa wakazi hao ambao ni jirani na mbuga hiyo wnapaswa kuyajali mazingira wanamo ishi kwa kyaweka katika hali ya kuvutia kwani mji wao unapokea wageni mbalimbali kutoka mataifa mbalimbali wanaokuja kutembelea mbuga hizo
Aktanabaisha kuwa siku ya uhifadhi duniani inasherehekewa duniani kote na hapa nchini imekuwa ikisherehekewa kwa kufanya shughuli mbalimbali za ujirani mwema kama tulivyofanya leo kufanya usafi wa mazingira kuzunguka kata ya mto wa mbu
Baadhi ya wananchi wa kata ya mto wa mbu wakiwa na wafanyakazi wa hifadhi ya ziwa Manyara wakishiriki kufanya usafi wa mazingira kwenye mji wa Mto wa Mbu ikiwa ni sehemu ya kusherehekea siku ya uhifadhi duniani
Usafi ukiendelea
Bango likihamsasisha usafi na utunzaji wa mazingira
Kila mtu bize
Bajaji likipakiwa takataka
Picha ya pamoja baada ya kusafisha kata ya Mto wa Mbu
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...