Rais Jakaya Mrisho Kikwete jana Jumapili Julai 6, 2014 alitembelea kwa mara ya pili maonesho ya kimataifa ya bishara katika viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam, baada ya ratiba yake kutokamilika katika ziara yake aliyoifanya siku ya Jumamosi kutokana na muda. Na kama ilivyo ada wananchi walifurahi kuwa naye karibu kama ambavyo yeye pia alifurahi kujumuika nao kwenye maonesho hayo ya kila mwaka. Watoto ndio waliokuwa wakimvutia zaidi Rais Kikwete ambapo kila mara alisimama na kuwasalimia.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya wananchi waliotembelea maonyesho ya Sabasaba.Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiteta na watoto aliokutana nao Sabasaba.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwaaga wananchi mara baada ya kujumuika nao pamoja kwenye Maonyesho ya Sabasaba jijini Dar. PICHA NA IKULU
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...